WANANCHI PWANI KUNUFAIKA NA 'SAMIA LEGAL AID':RC NYONGO

 


Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana nan Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani inaendelea kuratibu na kutekeleza Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Campaign).

RC Nyongo amesema Kampeni hiyo ina lengo la kusogeza huduma za msaada wa kisheria karibu na wananchi kuwaelimisha kuhusu haki na wajibu wao pamoja na kuwasaidia kupata ufumbuzi wa changamoto za kisheria zinazowakabili. 

Nyongo amesema hayo leo tarehe 23 Oktoba 2026 alipozungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika Ukumbi mdogo ofisini kwake Kibaha Mkoani Pwani. 

Amesema kupitia utekelezaji wa Kampeni wananchi wataendelea kuelimika kuhusu masuala ya umiliki na utatuzi wa migogoro ya ardhi, ndoa, mirathi na wosia haki za binadamu, ukatili wa kijinsia na kutatuliwa migogoro yao kupitia njia mbadala za utatuzi wa migogoro

Amesema kaulimbiu ya Kampeni hii inasema Msaada wa Kisheria kwa Haki ,Usawa, Amani, na Maendeleo ' ina akisi maono ya Dira ya Maendeleo ya taifa ya 2050 inayolenga kujenga jamii yenye usawa haki na ustawi wa wote.

RC Nyongo amesema utekelezaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria katika Mkoa wa Pwani ufunguzi rasmi utafanyika katika viwanja vya Stendi ya zamani Mailimoja Kibaha kuanzia saa tatu asubuhi baada ya ufunguzi Kampeni itatekelezwa kwa muda wa siku kumi kuanzia tarehe 29 Oktoba hadi 7 Novemba 2026.

Amesema kupitia utekelezaji wa Kampeni wananchi watapata fursa ya kupata ushauri na huduma za msaada wa kisheria kuwasilisha changamoto zao na kupata elimu kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria ikiwemo masuala ya ndoa na talaka mirathi na wosia ardhi na umuhimu wa utatuzi wa msaada wa kisheria. 

Aidha kupitia Kampeni wananchi wenye mashauri Mahakamani au katika vyombo vya utoaji haki watapata huduma za uwakili kupitia Mawakili wa Kujitegemea au Mawakili wa Serikali wakuidhinishwa kutoa huduma za msaada wa kisheria bure. 

 Wananchi wenye changamoto zinazohitaji utatuzi kwa njia mbadala wataalam wamewezeshwa mbinu za kutatua migogoro kwa njia mbadala .

Ametoa rai kwa wananchi watumie fursa hii adhimu kupata huduma za msaada wa kisheria bure.

"Kupitia Kampeni hii huduma zifuatazo zitatolewa bila malipo kwa wananchi ambazo ni ushauri wa kisheria, vilevile kutakuwa na huduma ya usajili wa matukio maalum ya binadamu ikiwemo usajili wa vyeti vya kuzaliwa na vifo RITA' amesema Nyongo.

RC Nyongo amesema kuwa utekelezaji wa Kampeni hii ni juhudi za serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha upatikanaji wa haki kupitia huduma za msaada wa kisheria kwa makundi yenye uhitaji zaidi hususan wanawake , watoto, wazee, watu wenye ulemavu na vijana .

Amesema kuwa ni matarajio yetu kwamba utekelezaji wa Kampeni awamu ya Pili Mkoa wa Pwani utawafikoa wananchi wengi huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 50%.

Post a Comment

0 Comments