RC Nyongo amesema hayo kufuatia malalamiko ya wananchi kukosa tiketi za kusafiria kutoka Mafia kwenda Nyamisati Mkoani Pwani
Amesema hivi sasa dunia imekua ya mtandao nimefika hata mimi Bandarini hii kero nimefanya mawasiliano na TEMESA nimewaeleza tutoke kwenye utaratibu wa kukata tiketi online.
Hili litekelezwe mara moja na wamesema mwisho wa mwezi huu utakamilika tuwe tunakata tiketi online kukata tiketi kwa utaratibu wa zamani huo ni wizi .
Mwananchi aliyejitambulisha kwa jina laa Hassan Shomari amesema leo unapotaka kusafiri inakulazimu usafiri uambali mrefu wa Km 54 kwenda bandarini safari huna tunaomba serikali tupate tiketi za online.
Mhe. Nyongo ametoa kauli hiyo leo, Novemba 7, 2026, alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kisiwani Mafia kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananchi.

Akijibu kero hiyo, RC Nyongo amewatoa hofu wananchi kwa kueleza kuwa kuanzishwa kwa mfumo wa tiketi za mtandaoni kuanzia mwezi ujao kutasaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo, kupunguza usumbufu na kuboresha safari za wananchi wa Mafia.
Awali, wakichangia katika mkutano huo, wananchi waliibua changamoto ya upatikanaji wa huduma za usafiri, hususan kivuko, wakieleza kuwa utaratibu wa sasa unawalazimu wasafiri kufika bandarini ili kuandika majina na kupata nafasi ya kusafiri.

Walisema hali hiyo imekuwa ikiwapa usumbufu mkubwa, ikiwemo baadhi ya wasafiri kukosa nafasi ya kupanda kivuko kutokana na kutokuwepo kwa mfumo rahisi wa kupata tiketi wakiwa walipo.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara Wilayani Mafia Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amewahakikishia wananchi na wakazi wa Wilaya ya Mafia kuwa kuanzia mwezi ujao, utaratibu wa upatikanaji wa tiketi za kivuko utaanza kufanyika kupitia mfumo wa mtandao ili kurahisisha huduma za usafiri kwa wananchi.

0 Comments