Mhe. Nyongo ametoa wito huo leo, Oktoba 15, 2026, akiwa katika Shule ya Msingi Magengo, eneo ambalo mkutano huo unatarajiwa kufanyika.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea Kongani ya Viwanda iliyo chini ya Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji (TISEZA), ambapo atakagua maendeleo ya ujenzi wa viwanda mbalimbali vinavyoendelea kujengwa katika eneo hilo.
Aidha, atafanya mkutano wa hadhara na wananchi, ambapo atazungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo ya Mkoa wa Pwani, hususan fursa za kiuchumi na kijamii, uwekezaji na upatikanaji wa ajira.
Ziara hiyo ni sehemu ya shughuli za Serikali za kuwasiliana na wananchi kuhusu maendeleo ya nchi na kuendeleza juhudi za kukuza uwekezaji na ustawi wa jamii.

0 Comments