Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo ametoa wito kwa wawekezaji kujiweka tayari kutoa misaada mbalimbali ya kuchangia waathirika endapo kutatokea madhara ya mvua ya El-Nino kama ilivyotabiriwa na wataalamu wa Hali ya Hewa.
RC Nyongo amesema "ndugu zetu hawa wanachangia jamii inayowazunguka hapa hivyo basi niendelee kutoa wito kwa viwanda vingine vilivyopo ndani ya Mkoa wa Pwani kuendelea kushirikiana na Serikali za Mitaa kuchangia maendele kwenye masuala mbalimbali ikiwemo afya elimu na barabara"
Kwahiyo niwaombe wawekezaji wengine anayetengeneza mashuka,anayetengeneza matenti, anayetengeneza vyombo anayetengeneza chochote awe tayari endapo hali hii ikitokea.
Aidha RC Nyongo amesema kuwa upanuzi wa Kiwanda cha Goodwill (Tanzania) Ceramic Co., Ltd kilichopo Mkiu, Wilaya ya Mkuranga, utaongeza ajira, mapato ya Serikali na kuimarisha uchumi wa Mkoa.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Xiaoming Xie, amesema kuwa upanuzi huo unatarajiwa kuongeza ajira za moja kwa moja hadi kufikia takribani 4,000, ikijumuisha ajira mpya 1,000, pamoja na fursa nyingine 15,000 zisizo za moja kwa moja.
Aidha, zaidi ya asilimia 90 % ya malighafi zinazotumika Kiwandani hapo zinapatikana nchini, huku Kampuni ikiendelea kukuza bidhaa za Made in Tanzania na kuchangia maendeleo ya jamiii.
Wakati huohuo RC Nyongo ametoa wito kwa vijana kutumia fursa za ajira, wananchi kulinda mali za wawekezaji na viwanda kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii.
Ameongeza kwa kusema kuwa Serikali itawasiliana na mamlaka husika kutafuta ufumbuzi wa changamoto za tozo za vigae katika masoko ya kikanda, ili kuimarisha ushindani wa bidhaa za Tanzania na kuvutia uwekezaji zaidi.












0 Comments