CCM HAIWEZI KUJENGWA KWA MAKUNDI ,MAGONVI:MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR

 

Makamu wa Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Hemed Suleman Abdullah amesema Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa kutoka tukianza na Mwenyekiti wetu pamoja na ngazi zote kutoka Mkoa hadi Shina lazima tuwe na umoja.

 Lazima tuwe na ushirikiano lazima tuwe na upendo
 katika kutekeleza majukumu yetu ya Chama katika Mkoa wetu.

Amesema bila umoja hatutakuwa na Chama imara kwenye Mkoa wetu wa Pwani bila ya upendo hatutakuwa na utekelezaji mwema mwema wa majukumu yetu na bila ushirikiano hatutafanikiwa katika utekelezaji wetu.

Viongozi wote tuwe ngazi ya Wabunge kwa Wabunge Wabunge na Madiwani Wabunge na Wenyeviti wa wa Wilaya Wabunge na Makatibu wa Wilaya na vilevile katika ngazi ya Kata na ngazi ya Wilaya na ngazi nyingine zote lazima tufanye kazi kama timu ya kukisimamia Chama chetu.
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kuachana kabisa na vitendo vya kuwa na makundi, magonvi na mivutano hali ambayo inayoweza kusababisha kubomoa misingi imara iliyoachwa na waasisi waliotangulia. 

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Hayo yamesemwa wakati akiwahutubia Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Pwani katika Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere uliopo eneo la kwa mfipa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

Makamu huyo wa pili wa Rais pia ndiye mlezi mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani ambapo pia ameahidi kushirikiana na viongozi na wanachama wa CCM katika kukijenga chama pasipo kuwa na makundi.

"Chama chetu ni chama ambacho ndiyo  kipo madarakani na kinapendwa sana na wananchi lakini hakiwezi kujengwa kwa makundi,makundi,wala mvutano, amebainisha Mhe. Abdulla 

Amesema hakuja Pwani kulea makundi bali amekuja kulea kundi la Chama Cha Mapinduzi. 

Pia ameendelea kusema kwamba viongozi wote lazima wafanye kazi kama timu katika kukisimamia Chama Cha Mapinduzi kwa kufuata Katiba, Kanuni na Miongozo mbali mbali ambayo ipo.

Makamu huyo wa Pili wa Rais amesema kwamba hakuna sababu yoyote ile ya kuvutana kwani kwa kufanya hivyo sawa na sumu itakayokiumiza Chama Cha Mapinduzi.

Katika hatua nyigine mempongeza amempongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha heshima ya Chama Cha Mapinduzi na kuwafanya Watanzania kuwa na hali ya amani na utulivu kwa Serikali yao.
 Nao baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Pwani wameahidi kumpa ushiriķiano mkubwa wa hali na mali mlezi wao ikiwa pamoja na kuyafanyia kazi maelekezo yote ambayo ameyatoa kwa ajili ya maslahi mapana ya chama.

Post a Comment

0 Comments