Aidha, Serikali imejenga jumla ya vyumba vya madarasa 1,889, vikiwemo 64 vya Elimu ya Awali, 809 vya Elimu ya Msingi na 1,016 vya Elimu ya Sekondari, pamoja na matundu ya vyoo, maabara, maktaba, mabwalo, mabweni na majengo ya utawala, sambamba na ukarabati wa miundombinu ya shule.Mkuu wa Mkoa Pia amesisitiza umuhimu wa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanandikishwa na wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2027 wanaripoti katika shule walizopangiwa.
Kwa upande wake Katibu tawala Mkoa wa Pwani Richard Kayombo shule hiyo imepata nafasi ya kipekee na kuwataka wanafunzi kutumia maabara hiyo kama nyenzo muhimu katika kuongeza tija kwenye masuala ya teknolojia.
Naye Mkurugenzi wa Taafisi ya Capital pay Foundation kwa upande wa Tanzania Isack Nchunda amesema maabara hiyo itawafanya wanafunzi kuwa wabuni katika teknologia za mifumo na kuahidi kuwa kwa wale watakaokuwa wabobezi wataweza kupata fursa za ajira katika taasisi hiyo.
Uzinduzi wa maabara hiyo ni sehemu ya ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo katika kuimarisha elimu na kuwawezesha wanafunzi kupata maarifa na ujuzi wa TEHAMA.








0 Comments