PILANOI MIPONYI NGAYOK

 

*Ni msichana wa kimasai kutoka kata ya Kakesio Ngorongoro* aliyejiunga na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine tawi la Arusha kusoma shahada ya utalii na ukarimu kwa mwaka wa masomo 2026/2027 na kupata *ufadhili wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.*

Pilanoi anasema kwamba akiwa Mtoto wa kike hatamani kuona wanawake wa kimasai wakiolewa wengi kwa pamoja na mwanaume mmoja Ila hutokea hivyo kwa sababu baadhi wanakuwa hawajasoma.

“Jitahidini kuwasaidia watoto wa kike ndani ya jamii ya kimasai,hatupendi kuolewa ndoa za mitala bali ni umaskini tu”,anasema Pilanoi mara baada ya kuwa miongoni mwa wanafunzi waliofadhiliwa na Ngorongoro mwaka huu wa Masomo.

*Pilanoi* amesema kuingia kwake Chuo Kikuu kumemfanya kufika Dar es salaam kwa mara ya kwanza na hivyo kusisitiza kuwa atasoma kwa nguvu zake zote ili huko siku za mbele aweze kuwatumikia watanzania.

Kauli ya Pilanoi inaungwa mkono na katibu wa baraza la wafugaji Ngorongoro *James Moringe* ambaye amesema elimu ndiyo msingi wa watoto wa kike na jamii ya wafugaji.

Post a Comment

0 Comments