KAYOMBO AOMBA USHIRIKIANO KUTEKELEZA MALENGO PWANI

 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Richard Marcellino Kayombo, amewaomba viongozi na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa kumpa ushirikiano katika kutekeleza kwa ufanisi majukumu aliyopewa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kayombo amesema vipaumbele vyake ni pamoja na kuandaa mazingira bora ya kupokea wanafunzi wa Kidato cha Kwanza mwaka 2028, kujiandaa kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za El Niño, pamoja na kuongeza mapato ya Serikali.


Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi, Kayombo amesisitiza umuhimu wa ushirikiano, weledi na uwajibikaji katika kuhakikisha malengo ya Serikali yanafikiwa na wananchi wanapata huduma bora.

Kwa upande wake, aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Pili Hassan Mnyema, amewataka watumishi kumpa ushirikiano Mhe. Kayombo na kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu, uzalendo, utiifu na uwajibikaji.

Post a Comment

0 Comments