Social Icons

Featured Posts

Thursday, May 3, 2018

IDDY MKWERA NA RAMADHANI SHAURI WAPIMA UZITO KWA KUZIPIGA KESHO TAIFA


Bondia Idd Mkwera akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa mei 4 katika uwanja wa ndani wa Taifa kushoto ni mpinzani wake Ramadhani Shauri Picha na SUPER D BOXING NEWS

Promota wa mchezo wa ngumi Evalist Ernest  katiakati akiwainua mikono juu bondia Ramadhani Shauri kushoto na Iddy Mkwera baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Ijumaa mei 4 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Promota wa mchezo wa ngumi Evalist Ernest  katiakati akiwainua mikono juu bondia Ramadhani Shauri kushoto na Iddy Mkwera baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Ijumaa mei 4 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS


Promota wa mchezo wa ngumi Evalist Ernest  katiakati akiwainua mikono juu bondia Ramadhani Shauri kushoto na Iddy Mkwera baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Ijumaa mei 4 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Promota wa mchezo wa ngumi Evalist Ernest  katiakati akiwainua mikono juu bondia Ramadhani Shauri kushoto na Iddy Mkwera baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika Ijumaa mei 4 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

BONDIA IDDY MKWERA AKIPIMA AFYA KWA DR DOLNAD MADONNO KWA AJILI YA MPAMBANO WAKE NA RAMADHANI SHAURI


Bondia Idd Mkwera akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake wa mei 4 katika uwanja wa ndani wa Taifa kushoto ni mpinzani wake Ramadhani Shauri Picha na SUPER D BOXING NEWS

KOCHA SUPER D AZUNGUMZIA MPAMBANO WA SHAURI NA MKWERA


Kocha wa kimataufa wa mchezo wa masumbwi nchini Mhamila Rajabuakizungumza na wana habari kuhusu mpambano wa Ngumi kati ya Iddy Mkwella na Ramadhan Shauri utakaofanyika kesho mei 4/5/2018 katika uwanja wa ndani wa taifa indoor stadium

Kocha wa kimataufa wa mchezo wa masumbwi nchini Mhamila Rajabuakizungumza na wana habari kuhusu mpambano wa Ngumi kati ya Iddy Mkwella na Ramadhan Shauri utakaofanyika kesho mei 4/5/2018 katika uwanja wa ndani wa taifa indoor stadium
i

Monday, April 23, 2018

SUPER D AMNOWA IDD MKWERA KUMKABILI SHAURI MEI 5 UWANJA WA NDANI WA TAIFA


Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimnowa bondia Idd Mkwera kulia kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika mei 4 mwaka uhu utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa Mkwera atazipiga na Ramadhani Shauri mpambano wa raundi 10 Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akipambana na Idd Mkwera kushoto wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Ramadhani Shauri utakaofanyika mei 4 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi kumi Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Idd Mkwera akionesheana umwamba wa kutupiana makonde nma Ibrahimu Class 'king Class Mawe' wakati wa mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Ramadhani shauri utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa Mei 4 mwaka uhu Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Kelvin Majiba kushoto akipambana na Idd Mkwera wakati wa mazoezi ya Mkwera akijiandaa na mpambano wake na Ramadhani Shauri utakao fanyika mei 4 katika uwanja wa ndani wa Taifa 'INDOOR STADIUM' Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Kelvin Majiba kushoto akipambana na Idd Mkwera wakati wa mazoezi ya Mkwera akijiandaa na mpambano wake na Ramadhani Shauri utakao fanyika mei 4 katika uwanja wa ndani wa Taifa 'INDOOR STADIUM' Picha na SUPER D BOXING NEWS

VICENT MBILINYI AJINOWA KUMKABILI HUSSEIN SHEMDOE MEI MOSIKocha wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimnowa bondia vicent Mbilinyi kwa kumuelekeza kupiga ngumi ya mkunjo wa chini 'Upcat' Mbilinyi anajiandaa na mpambano wake na Hussein Shemdoe utakaofanyika katika ukumbi wa musoma Bar siku ya Mei Mosi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu

BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea na mazoezi ya kumkabili Hussein Shemdoe wakati wa mpambano wao utakaofanyika mei mosi siku ya sikukuu ya wafanyaklazi Dunian mpambano uho utafanyika katika ukumbi wa Musoma Bar uliopo Tandika Mwembe Yanga mpambano wa raundi 8

Mbilinyi anaenolewa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amekuwa nje ya ulingo kwa mda wa mwaka mzima sasa tangu mwishoni mwa mwaka 2016 na sasa anakuja kivingine

mbali na mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia mbali mbali ambapo bondia Shafii Ramadhani atapambana na Antony Mathias wakati Nassibu Ramadhani atavaana na Hamisi Mohamedi na Shomari Galibu atapambana na Hashimu Sheni wakati Said Mlugulu atavaana na Said Bakari 'Kidedea' 

Mapambano haya yoteyatafanyika siku hiyo katika ulingo mpya  wa mdau wa masumbwi nchini Zahoro Maganga 'Super Diego' aliejenga ulingo uho kwa ajili ya kuwakombowa mabondia na hadha ya kupigania chini 

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani

Friday, April 13, 2018

MABONDIA KUONESHANA UMWAMBA MEI 5 IDD MKWERA NA RAMADHANI SHAURI KUWAONGOZA

Na Mwandishi WetuBondia Idd Mkwera baada ya kupoteza mpambano wake wa nje uliofanyika Riga Ratvia kwa point bondia huyo sasa amesaini mkataba wa kuzipiga na bondia machachari Ramadhani Shauri mpambano wa raundi 10 utakaofanyika Mei 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa

akizungumza wakati wa utaiaji saini uho Mkwera amesema kuwa yeye anachojua ngumi ndio kazi yake hivyo kwake kazi ni kazi tu aijalishi anacheza na nani hivyo kuwataka wapenzi wa mchezo wa masumbwi kuja kushudia mpambano uho wa masumbwi siku hiyo

akijibu mapigo Shauri amesema wapenzi wangu na mashabiki zangu mmenikosa tangu mwaka jana nilivyopoteza kwa pointi katika uwanja ule ule sasa nilitoka kidogo nje ya Tanzania hivyo nimerudi na kasi mpya nguvu mpya njoeni mshidie ngumi zinavyopigwa

Nae Promota wa mchezo huo Evalist Ernest alisisitiza kwa kusema mabondia hawa watacheza mpambano wa raundi 10 katika uzito wa kg 62.5 hivyo muje mushudie masumbwi siku hiyo mbali na mpambano uho siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi kwa vijana tulio wasainisha

siku hiyo bondia Haidari Mchanjo atazichapa na Amani Bariki 'Manny Chuga' wakati Karimu Ramadhani atakumbana na Jerms Kibazange   na Said Chini ataoneshana umwamba na Hamza Mchanjo

Mapambano hayo na mengine yote yatakuwa wakisindikiza pambano kuu kati ya Idd Mkwera na Ramadhani Shauri watakaozipiga Raundi kumi 

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani
Promota wa mpambano wa ngumi Evalist Ernest katikati akiwainua mikono juu mabondia Iddi Mkwera kushoto na Ramadhani Shauri baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Mei 5 katika ukumbi wa Uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi kumi Picha na SUPER D BOXING NEWS

MABONDIA IDD MKWERA NA RAMADHANI SHAURI WASAINI KUZIPIGA MEI 5 UWANJA WA NDANI WA TAIFA


Promota wa mpambano wa ngumi Evalist Ernest katikati akiwainua mikono juu mabondia Iddi Mkwera kushoto na Ramadhani Shauri baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Mei 5 katika ukumbi wa Uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi kumi Picha na SUPER D BOXING NEWS
Promota wa mpambano wa ngumi Evalist Ernest katikati akimkabidhi mkataba wake bondia Idd Mkwera baada ya kutiliana saini ya kuzipiga na Ramadhani Shauri kulia mpambano utakaofanyika mei 5 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Idd Mkwera akizungumzia mpambano wake wa mei 5 mwaka uhu atakapozipiga na Ramadhani Shauri kulia katikati ni Promota wa mpambano wa ngumi Evalist Ernest Picha na SUPER D BOXING NEWS

Promota wa mpambano wa ngumi Evalist Ernest katikati akiwatambulisha mabondia Haidar Mchanjo kushoto na Amani Bariki 'Manny Chuga' baada ya kusaini kuzipiga mei 5 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Said Chino kushoto akitambiana na Hamza Mchanjo baada ya makubaliano ya kuzipiga mei 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Karimu Ramadhani kushoto akitambiana na Jems Kibazange baada ya makubaliano ya kuzipiga mei 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS

Thursday, April 5, 2018

RAIS MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZA POLISI ARUSHA APRILI 7


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pohn Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa nyumba za polisi na vituo vya polisi Jijini Arusha.

Akizungumza na waandishi wahabari Kamanda wa polisi jijini hapa DCP Charles Mkumbo amesema kuwa kutakuwa na uzinduzi wa vituo viwili cha Utalii na Diplomasia na kingine ni Kituo cha daraja la kati kilichopo Murieti Jijini Arusha.

Kamanda Mkumbo amesema kuwa kutakuwepo pia na maonyesho mbalimbali ya jinsi Jeshi la Polisi linavyofanya kazi za kuwahudumia wananchi ambapo maonyesho hayo yatafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid .

Amewataka wananchi kutokuwa na hofu kwani hali ya usalama Jijini hapa 
umeimarishwa na amewaomba wajitokeze  kwa wingi katika sherehe hizo.
Kituo chaPolisi cha   Utalii na Diplomasia kinachotarajiwa kuzinduliwa April 7 Jijini Arusha.Picha na Vero Ignatus Blog.
Baadhi ya Nyumba za Polisi zinazotarajiwa kuzinduliwa na Mh.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli

Sunday, March 25, 2018

WAZIRI UMMY AMTAKA DED TANGA KUTENGA ENEO KWA AJILI YA TAASISI YA GIFT OF HOPE INAYOSIMAMIA KITUO CHA SOBBER HOUSE


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katika akimkabidhi pikipiki Mkurugenzi wa Kituo cha Sober House cha Gift of Hope kilichopo Kange Jijini Tanga Saidi Bandawe kwa ajili ya kuitumia kwenye matumizi yao


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akizungumza mara baada ya kukabidhi pikipiki hiyo

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM)katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi ambao waliambatana nae ikiwemo vijana matibabu ya kuachana na matumizi ya dawa za kulevya.

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutenga eneo la hekari 10 kwa ajili ya Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Gift of Hope Foundation ambayo inasimamia kituo cha Sober House.

Hayo ameyazungumza alipotembelea kituo hicho kinachow asaidiawaat hirika wa madawa ya kulevya kilichopo eneo la Kange kata ya Maweniambapo alikabidhi pikipiki 1 kwa ajili ya kituo hicho.

Waziri Ummy alisema jambo linalofanywa na taasisi hi yo lazima liungwe mkono na Serikali kutokana na jitihada zao za kukabiliana na mapambanoya matumizi ya madawa ya kulevya hasa kwa waathirika.

Alisema nguvu kubwa inatumiwa na waanzishaji wa nyumba hizo kwa lengola kusaidia vijana huku wakikosa msaada wa kudumu wa kuwawezeshawaweze kujitegemea tofauti na ilivyo sasa wanavyoishi kwa kuomba misaada.

“Jambo linalofanywa hapa sobber house ni juhudi kubwa na lazima sis ikama serikali tuwaunge mkono hawa watu wakishindwa makundi haya kama yatarudi mitaani hali inaweza kuwa mbaya zaidi”Alisema.

Aidha alisema kufuatia taarifa ya taasisi hiyo ya kuhitaji eneo la
kutosha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba,shughuli za mikono ikiwamou fugaji,kilimo cha mbogamboga na hata ufundi ni jambo la msingi naviongozi wote wanatakiwa walione kwa jicho la tatu.

“Jamani hawa watu wasiishi kw a kuombaomba lazima wapatiwe eneo lao na waanzishe miradi yao itakayowasaidia kujikimu na mahitaji ya kila sikuna tukifanya hivi tutaokoa kundi kubwa la vijana linaloangamia sikihadi siku”Alisema Waziri Ummy.

Mbali na hilo alisema akiwa kama Waziri mwenye dhamana atahakikisha dawa za Methadol zinafika Moani hapa kama ilivyo katika mikoa mingine ili kuweza kuwasaidia vijana hao kupunguza makali ya madawa.

“Kwanza nashangaa kama tanga haipati dawa hizi za methadol ikiwa ni mkoa wa pili baada ya dare s salaam kwa wingi wa watumiaji wa mada ninayo dhaama na dawa hazi zitafika sasa kwa ajili ya vijanawetu”Alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa taasisi hiyo Said Bandawe alisema kwasasa wanaishi katika nyumba ya kupanga na wamepewa eneo na wamepewa eneo la mtu kwa kuazimwa kwa ajili ya kilimo cha mbogamboga nashughuli za ufugaji.

Alisema maisha ya vijana  bado magumu hasa swala la chakula,malazi,dawa za Methadol, na namna ya kupata mahitaji ya kila siku kwa ujumla huku akijaribu kutafuta mahitaji kwa kuomba misaada kuwasaidia vijana haowanaokadiriwa kufikia 68 (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

DJ LUKE RAIS WA JUMUIYA YA WATANZANIA WDMV 2018

Matokeo ya Uchaguzi wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Lucas Mukami (DJ Luke) ameibuka kuwa mshindi wa Urais wa Jumuiya ya Watanzania DMV kwa kura kupata idadi ya 315, dhidi ya Liberatus Mwang'ombe, aliyepata kura 262. akifuatiwa na Rebeca 24.
Nafasi ya Makamu wa Rais imechukuliwa na Joha 352 Joyce 248. Katibu ni  Cleopatra 311 Omby 214 Dotto 70. Katibu  Msaidizi Saria 360 DMK 23. . Mweka Hazina msaidizi ni Magret 263 Mikidadi 329.... Bodi inaundwa na  na Mashaka 413 Zena 296 Jabil 330. Pius 454 Asha 386 Hamza 295 Ruth 250.

Thursday, March 22, 2018

WCF YAWAELIMISHA MAAFISA WAAJIRI KUHUSU MISINGI YA KULINDA USALAMA NA AFYA ZA WAFANYAKAZI MAHALA PA KAZI


 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, (aliyesimama), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina juu ya masuala ya msingi ya kulinda usalama na afya mahala pa kazi na Fidia kwa wafanyakazi kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, (JNICC), jijini Dar es Salaam Machi 22, 2018. Wengine pichani  I Mkurugenmzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, (katikati), na Meneja wa Tathmini ya hatari mahala pa kazi, (Workplace Risk Assesment Manager), Bi. Nanjela Msangi.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

NIWAJIBU wa mwajiri kutoa taarifa kwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ya kuumia kwa mfanyakazi wake ikiwa ni pamoja na kifo.

Hayo yamesemwa leo Machi 22, 2018, na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Anselim Peter, wakati akifungua semina ya siku moja iliyowaleta pamoja mameneja na maafisa waajiri kutoka sekta ya umma na binafsi jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Wafanyakazi, (JNICC), jijini Dar es Salaam.

Pia ni wajibu wa mwajiri kumpatia vifaa vya kujilinda (protective gears), mfanyakazi wake,  kulingana na kazi anayofanya ili kumlinda na madhara yatokanayo na kazi anayofanya.

“Lengo la Mfuko sio tu kusajili waajiri na kupokea michango lakini pia ni kukuza mbinu za kuzuia ajali, magonjwa ama vifo katika maenmeo ya kazi na ndio msingi mkuu wa seemina yetu ya leo, katika kutekeleza jukumu letu hili ni kujenga uelewa wa kutosha kwa mwajiri ili kuhakikisha kwamba tunajenga mazingira ya kuzuia ajali sehemu za kazi.” Alisema na kuongeza.
Nia ya Mfuko ni kuona tunakinda nguvu kazi ambapo tunahakikisha kwamba wafanyakazi hawa wawapo kazini hawaugui au kuumia au kufariki kutokana na kazi, alissisitiza Bw. Peter.
Alisema washiriki watapatiwa mafunzo mbalimbali yanayolenga kujenga mazingira mazuri kwa wafanyakazi wawapo kazini. “Mtaelimishwa kuhusu masuala muhimu kuhusu Mfuko kupitria mada mbalimbali zitakaziowasilishwa na wataalamu, kutekeleza vyema jukumu la kuhamasisha na kusisitiza wafanyakazi kuzingatia kanuni za kulinda usalama mahala pa kazi, masuala ya fidia kwa wafanyakazi, wanaoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi.” Alifafanua.
Alisema, uwepo wa Mfuko umeleta faraja kubwa kwa waajiri na wafanyakazi ambapo leo hii, endapo Mfanyakazi atapata madhara kutokana na kazi, anao uhakika kuwa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, utatoa fidia stahili kulingana na mikataba ya kazi na mwajiri husika.
“Yote haya yanawapa wafanyakazi utulivu wawapo kazini kwani wanajua kuwa lolote likitokea ipo taasisi ambayo itasimamia na kunifidia nah ii inaondoa migogoro sana sehemu za kazi.” Alisema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar alisema Mwajiri anao wajibu wa kumuwekea mazingira bora, salama na yana afya ili aweze kufanya kazi kwa ufanisi. “Sio tu kupewa mazingira mazuri lakini pia apewe vifaa kinga kitaalamu vinaitwa personal protective equipmentskwa kufanya hivyo utakuwa unalinda usalama wake na afya yake.” Alisema Dkt. Omar.
“Mfanyakazi anayo haki ya kumdai mwajiri wake kumpatia vifaa vya kujilinda na mwajiri haruhusiwi kumfukuza kazi au kumwadhibu mfanyakazi anayedai mazingira bora toka kwa mwajiri wake ili aweze kuwa amekingwa.” Alifafanua.
Pia alisema mfanyakazi naye anao wajibu kuvitumia vifaa vya kujikinga katika mazingira yake ya kazi kwa usahihi na wakati wote awapo kazini.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa semina hiyo, BwAlly Kinga Shamte, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Badri East Africa Enterprises, mesema tayari kampuni yake imeanza kufaidika na kujiunga na Mfuko huo ambapo mmoja wa wafanyakazi wake, aliyepata shoti ya umeme ameweza kushughulikiwa na Mfuko na tayari anahudumiwa.
“Hii imekuwa ni kama Bima kwa wafanyakazi wetu, sisi hatushughuliki tena na madhara anayopata mfanyakazi, tulichofanya ni kujaza fomu zao za taarifa ya ajali hiyo na mara moja walianza kumshuhhulikia.” Alisema.

 
 Mshiriki akisoma machapisho yenye taarifa za WCF
 Dkt. Abdulsalaam (katikati), akifafanua baadhi ya hoja. Wengine, ni Bi. Naanjela Msangi, (Kushoto), na Bw. Faustine George
 Bi. Naanjela Msangi.
 Bw. George Faustine, Afisa Matekelezo-WCF
George Faustine, Afisa Matekelezo-WCF
  Bi. Naanjela Msangi(kulia), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano WCF, Bi. Laura Kungenge
 Baadhi ya washiriki wakijadiliana jambo
 Baadhi ya washiriki wakipitia vipeperushi vyenye maelezo kuhusu kazi za Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
 Baadhi ya washiriki wa semina.
 Washiriki wakijiandikisha
 Washiriki wa semina wakifuatilia mada mbalimbali kutoka kwa wataalamu wa WCF.
 Robert Duguza, Afisa wa usalama na afya mahala pa kazi, akizungumza wakati wa semina hiyo.


Bi. Tumaini J.Kyando, Afisa Mwandamizi wa Afya na Usalama mahala pa Kazi kutoka Mfuko w aFidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio walioandaa semina hiyo, akinakili baadhi ya hoja zilizojitokeza.
Baadhi ya washiriki
 
 
Blogger Templates