Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imewataka watumishi wake waliohudhuria mafunzo ya kiutumishi kwa siku tano mjini Dodoma kuyafanyia kazi mafunzo yao ili waweze kuongeza ufanisi katika utendaji.
Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo anayeshughulikia huduma za shirika Aidan Makalla ametoa rai hiyo kwa watumishi has wakati akifunga mafunzo ya wiki moja yenye lengo la kuwajengea watumishi uelewa kuhusu utawala bora, usimamizi wa rasilimali watu, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika uhifadhi, Utoaji wa huduma bora kwa wateja na nidhamu mahala pa kazi
Makalla amesema mamlaka imewekeza mtaji kwa watumishi hao kwa kuwapa elimu hiyo ya utumishi, maadili, uwekezaji,afya ya akili na itifaki ikiamini kwamba mafunzo ndiyo nyenzo muhimu katika uwajibikaji.
“Sisi viongozi wa mamlaka ni kama wazazi tuna wajibu wa kuwapa mafunzo ili msiharibikiwe na baadaye mamlaka ikaja kulaumiwa, yatumieni mafunzo haya kuyajenga katika kazi zenu,”alisema Makalla.
Hii ni awamu ya Pili kwa mwaka huu wa fedha kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutoa mafunzo kwa watumishi wake ikiamini kwamba asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu.

0 Comments