KUNDI LA KANGA MOKO YATAITIWA BUNGENI


KIKUNDI cha unenguaji cha wasichana jijini Dar es Salaam maarufu kama kanga moto, ndembendembe, laki si pesa, jana kiliibua gumzo bungeni wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ambapo baadhi ya wabunge walisema kinapotosha maadili ya Utanzania.

Mbunge wa Viti Maalum, Mwanamrisho Taratibu Abama (Chadema), ndiye alikuwa wa kwanza kulizungumzia kundi hilo huku akiihoji serikali ni kwanini imekaa kimya wakati utamaduni ukipotoshwa kwa kuchochea ngono.

Mbunge huyo aliungwa mkono na mbunge mwenzake wa viti maalum, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM), ambaye alifafanua kuwa mbali na kuvaa kanga hiyo moja bado vazi hilo hulowanishwa maji na kasha kungua ili mauongo yao yaonekane.

“ Mheshimiwa Spika watu wanafurahia na wanakwenda kuwatazama, lakini mimi naona huko ni kumomonyoa maadili yetu, hiwezekani watu wafanye hivyo halafu tuwashingile wakati wanapotosha na kutamaisha wengine kingono,” alisema.

Wabunge hao pia walilalamikia hatua ya serikali kufumbia macho filamu za ngono zinzaouzwa hovyo mitaani na wakati mwingine kuwekwa picha za wasanii wa Tanzania wakati ndani wanaonekena watu wengine.
Abama alisemakuwa inashangaza kuona serikali haiwazui wasanii wamotengeneza filamu za ngono, usagaji na ushoga na kasha kuzismabaza mitaani.

Kwa upande wake mchungaji Rwakatare, alilaumu vituo vya redio na televisheni kutumia muda mwingi kupiga miziki na kurusha filamu za kimagharibi na matangazo wakati vikitoa muda mfupi kwa taarifa za habari ambazo ndizo muhimu kwa wananchi.

“Taarifa za habari zinapaswa kurushwa kwa kirefu na kurudiwa mara kwa mara ili watu waelewe. Maana kwa mujibu wa wataalamu ili mtu aweze kuelewa ni lazima asikie mara 16,” alisema mchungaji Rwakatare.

Post a Comment

0 Comments