DACHI NA CHUMA WAWASHA MOTO


Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro na Shirika la Utangazaji Tanzania ( TBC) zimejipanga kuendeleza ushirikiano wa kutangaza vivutio vya Utalii vilivyopo Ngorongoro kupitia utalii wa michezo kuelekea mashindano ya AFCON mwaka 2027

Akifungua mafunzo maalum ya Watangazaji wa mpira wa miguu wa redio za Shirika la Utangazaji Tanzania yaliyofanyika Ukumbi wa NCAA Karatu, Mkurugenzi Mkuu wa TBC Asha Dachi ameeleza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwaongezea maarifa na ujuzi wa kitaaluma ili kuboresha utangazaji wa michezo na kuiunganisha na Sekta ya Utalii

Ameeleza kuwa Vyombo vya habari vina dhima kubwa kuelimisha umma kupitia michezo na vivutio vya utalii vilivyopo nchini hivyo kupitia mafunzo hayo watapata fursa ya kutembelea Ngorongoro na makumbusho ya Urithi Geopark ili kujifunza zaidi vivutio vya utalii vilivyopo na kuviingiza katika matangazo ya program za Michezo kuelekea mashindano ya AFCON mwaka 2027 ambapo Tanzania ni sehemu ya nchi wenyeji. 

Kwa upande wake Kamishna msaidizi mwandamizi anayesimamia huduma za  Utalii na masoko Ngorongoro Mariam Chuma Kobelo ameeleza kuwa Ngorongoro itaendeela kuwa bega kwa bega na  TBC  ili kutangaza maajabu ya  vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro, uboreshaji wa miundombinu ya utalii, huduma zinazotolewa Ngorongoro na fursa za uwekezaji kwa ajili ya kuzinadi kwenye matukio mbalimbali ya kimataifa yanayofanyika nchini.

Post a Comment

0 Comments