Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo leo amesema kuwa ameridhishwa na hali ya uwekezaji alipotembelea eneo la Kongani ya Viwanda Kwala Kibaha Vijijini .
RC Nyongo amesema hayo leo tarehe 21 Oktoba 2026 alipokua katika ziara kwenye eneo hilo la Kongani ya eneo la Kwala ambayo inayomilikiwa na na watu binafsi
"Tunafahamu kwamba kongani zingine zinamilikiwa na Serikali chini ya Taasisi ya TISEZA, Kongani hii ni kubwa na wamekaribisha wawekezaji wengi kuna baadhi ya Kampuni wamejenga viwanda na wamekwisaha anza uzalishalji" amesema RC Nyongo.
Amesema sisi kama serikali ya Mkoa leo tumewaahidi tunakwenda kuzifanyia kazi changamoto zao ikiwemo umeme ambapo Shirika la Umeme TANESCO wameahidi kwamba wanatengeneza kituo cha kupoza umeme Chalinze.
Amesema kuwa tumewalekeza wapunguze bei kwa wawekezaji wanaotoka nje ya nchi ili waje wawekeze sababu wakiweka bei kubwa gharama za uzalishaji zinaongezeka wawekezaji wengine wakipiga hesabu wanaweza wasije.

Mhandisi Mkuu wa Shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Pwani Issack Kwigema amesema ujenzi wa miundombinu ya umeme hasa ukiangazia athari zinazoweza kutokea katika kipindi cha mvua utaweza kuona kwa sasa tubabadilisha nguzo za miti na kuweka za zege.
Amesema tuko katika kipindi cha mwezi mmoja kutoka sasa mpaka Novemba 30 hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo ya makazi na maeneo ya viwanda yatastahikilika na kuimarika vizuri.
Amesema hayo leo tarehe 21 Oktoba 2026 wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kituo kipya cha kupokea na kupoza umeme msongo wa Kilovoto132/33 kilichopo Mlandizi Wilayani Kiabaha Mkoani Pwani.
hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo amesema maeneo mengi ambayo yalikuwa yanapata umeme kwa kutumia nguzo za zamani sasa hizo laini zinarekebishwa.
RC Nyongo amesema nguzo hizo zinarekebishwa ili endapo mvua za El-Nino zitakapoanza kunyesha pia ikumbukwe zinatishia kuwa na mafuriko, wananchi watapata umeme wa uhakika.
Aidha Nyongo amesema kuwa atahakikisha anafuatilia kwa karibu utekelezaji wa utoaji wa huduma bora ya umeme wa uhauhakika
Katika hatua ingine Mkuu wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo amesema kuwa ameridhishwa na hali ya uwekezaji alipotembelea eneo la Kongani ya Kwala Kibaha Vijijini .
RC Nyongo amesema leo tumefika hapa Kongani ya eneo la Kwala ambayo ni Kongani inayomilikiwa na na watu binafsi.
Tunafahamu kwamba kongani zingine zinamilikiwa na Serikali chini ya Taasisi ya TISEZA, Kongani hii ni kubwa na wamekaribisha wawekezaji wengi kuna baadhi ya Kampuni wamejenga viwanda na wamekwisaha anza uzalishalji.
Ujenzi wa Kituo hiki umegharimu kiasi cha TSHS.16Bil. na umetekelezwa chini ya Mkandarasi TBEA Limited
Wakati huoho ameongeza kwa kusema kuwa Kituo hiki kinapokea umeme wa Msongo wa Kilovoti 132 kutoka Ubungo na Chalinze na kupoza hadi Kilovoti 33 kwa ajili ya usambazaji kwa wateja ,Kituo hiki kina Transfoma mbili mpya zenye uwezo wa MVA 60 kila moja sawa na NW 110 pia kina njia 11(Feeders) za usambazaji wa huduma ya umeme kwa wateja
Amesema sisi kama sisi kama serikali ya Mkoa leo tumewaahidi tunakwenda kuzifanyia kazi changamoto zao ikiwemo umeme ambapo Shirika la Umeme TANESCO wameahidi kwamba wanatengeneza Kituo cha kupoza umeme Chalinze.
Amesema kuwa tumewalekeza wapunguze bei kwa wawekezaji wanaotoka nje ya nchi ili waje wawekeze sababu wakiweka bei kubwa gharama za uzalishaji zinaongezeka wawekezaji wengine wakipiga hesabu wanaweza wasije.
Mhandisi Kwigema amesema kuwa Mkuu wa Mkoa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Ufaransa kupitia Shirika la Maendeleo AFD inatekeleza miradi ya ukarabati na uboreshaji wa Gridi ya Taifa ambapo Kituo Cha Mlandizi ni miongoni mwake.
"Kituo hiki kwa sasa kinahudumia maeneo ya Kibaha Vijijini, Chalinze,
Àmesema kuwa Kisarawe na Bagamoyo huku kukiwa na maeneo nyeti kama vile mitambo yote ya maji Ruvu Juu na Ruvu Chini,Hospitali ya Wilaya ,Bandari Kavu, Kwala na Kambi ya Jeshi Ruvu.
Mha.Kwigema amesema lengo la ujenzi wa Kituo hiki ni kuimarisha huduma ya upatikanaji umeme katika maeneo ya Kibaha Vijijini,Bagamoyo, Chalinze, na hasa eneo la Viwanda Zegerenj na Zogowale Mkoani Pwani.
Aidha amesema kuwa ujenzi huu wa Kituo unauwezo wa kupokea na kupooza umeme cha Mlandizi, utekelezaji wake ulianza Januari Mosi 2023 na umekamilika kwa asilimia 100% Septemba 30 ,2026.
0 Comments