NI MWENDO WA KUWAVURUGA WANYAMA PORI WAKALI NA WAHARIBIFU

 

Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la *Ngorongoro* (NCAA) tarehe 3 Novemba, 2026, imekabidhi Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kituo cha mwitikio wa haraka kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu kilichojengwa katika Kijiji cha Naalarami, Wilaya ya Monduli, Mkoani Arusha.
Akizungumza wakati wa kukabidhi kituo hicho Naibu Kamishna wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za Shirika Ngorongororo Aidan Makala amesema kuwa ujenzi wa vituo vya askari wa wanyamapori kwa ajili ya kutoa muitikio wa haraka kwa matukio yanayohusisha wanyamapori wakali na waharibifu ni sehemu ya mchango wa Mamlaka katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kukabiliana na changamoto hiyo.

Amesema lengo la Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia taasisi zake ni kuimarisha usalama wa wananchi, ambapo tayari Ngorongoro imejenga vituo hivyo Monduli, Babati, Same, Korogwe na Rufiji.

Msimamizi wa Ujenzi wa Kituo hicho Mhandisi Faraja Sembua ameeleza kuwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho uliofanyika kwa kipindi cha miezi mitano na kugharimu shilingi milioni 102 ambapo kituo kinajumuisha ofisi, vyumba vya kulala, na sehemu za kuhifadhi silaha, choo na bafu pamoja na miundombinu mingine muhimu.

Akipokea kituo hicho Kamishna Msaidizi Mwandamizi kutoka TAWA P.M Kasisi ametoa shukrani kwa Ngorongoro kuunga mkono juhudi za kudhibiti migangano ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa mali za wananchi na kuahidi kusimamia kituo hicho ili kiwe na manufaa kwa wananchi .

Post a Comment

0 Comments