Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani imekutana na wadau wa Forodha, hususan wafanyabiashara wanaojihusisha na uingizaji na usafirishaji wa mafuta ya kupikia kupitia Bandari ya Bagamoyo, kwa lengo la kusikiliza changamoto zao na kutafuta ufumbuzi wa pamoja utakaowezesha shughuli za biashara kufanyika kwa ufanisi.
Kikao hicho kilichofanyika tarehe 20 Oktoba 2026, katika ofisi za TRA Wilaya ya Bagamoyo, kimekuwa sehemu ya jitihada za TRA kuimarisha mawasiliano na wadau wa Forodha, kutambua changamoto zinazowakabili na kujadili hatua za kuzitatua ili kuboresha mazingira ya biashara.
Akizungumza katika kikao hicho, Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani, Bw. Peter Jackson, amesisitiza kuwa TRA inaendelea kusimamia sheria na taratibu za Forodha huku ikiweka mazingira wezeshi kwa biashara halali. Ameeleza kuwa udhibiti wa bidhaa za magendo unafanyika kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Serikali, na kusisitiza umuhimu wa kutoa elimu ya kodi na Forodha kwa wafanyabiashara.



0 Comments