PWANI KUZINDUA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA MAMA SAMIA


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari  Kunenge amesema kuwa Mkoa wa Pwani utazindua  Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama  Samia 'Samia Legal Aid' tarehe 24 Februari 2025 katika Viwanja vya Stendi ya zamani Mailimoja Kibaha. 

RC Kunenge amesema hayo leo tarehe 22 Februari  2025 kwenye mkutano  na Waandishi wa Habari uliofanyika ofisini kwake Mkoani hapa. 

Kunenge ametoa wito kwa wananchi   wa Mkoa wa Pwani  kujitokeza kwa wingi  kesho Jumatatu kuanzia  saa tatu asubuhi.

"Wananchi wote wenye  malalamiko  wajitokeze kupeleka malalamiko yao yanayohitaji msaada  kisheria  na nina imani watapata msaada" amesema  Kunenge.

Amesema kuwa kwa malalamiko  yote yanayohusiana  na masuala na ndoa , mirathi, ardhi  wote watasikilizwa

Huduma hii inatolewa na Wizara ya Katiba  na Sheria.

Tayari  Kampeni  ya Msaada  wa Kisheria  ya Mama Samia  imefanyika kwenye Mikoa 19 na Pwani unakua Mkoa wa 20.

Post a Comment

0 Comments