MIMEA VAMIZI NI TISHIO KWA IKOLOJIA YA HIFADHI ZETU, BALOZI POLEPOLE

Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humprey Polepole amesema uwepo wa mimea vamizi katika maeneo yaliyohifadhiwa inaathiri na  kubadilisha ikolojia ya maeneo hayo hali ambayo inapelekea kutoweka kwa nyanda za malisho ya Wanyamapori. 

Mhe. Balozi Polepole aliyasema hayo leo tarehe 19 Februari, 2025 katika tambarare za Ndutu baada ya kuungana na timu ya watafiti kutoka Cuba na Tanzania wanaondelea na ziara yao ya kitafiti kuhusu mimea vamizi ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

Aidha Mhe. Balozi Polepole alieleza kuwa maelekezo ya Serikali ni kutafuta suluhu ya kudumu ya mimea vamizi huku ikilenga kubadilisha mimea hiyo kupata bidhaa ambazo  ni rafiki kwa matumizi ya binadamu ikiwemo  mimea dawa (Medicinal plants).

Hata hivyo mimea vamizi ambayo imeonekana na watafiti hao ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ni pamoja na Parthenium hysterophus (Gugu karoti, Gutenibergia cordifolia (Gutenbergia).

Watafiti hao wamehitimishwa ziara yao katika Hifadhi ya Ngorongoro ambapo timu ya watafiti hao walitembelea baadhi  ya maeneo ya  Kayapus, Kakesio na Tambare za Ndutu.

Post a Comment

0 Comments