BAADA ya
kukaa nje ya gemu la muziki kwa miaka miwili leo usiku mwanamuziki wa kike na
asiye na mpizani Rehema Chalamila ‘Ray C’ anatarajiwa kutoa burudani yake
katika shindano la kumsaka Redds Miss Ilala 2013 litakalofanyika katika ukumbi
wa Diamond Jubilee Agosti 16 imefahamika.
Mbali ya
Ray C burudani zingine zitatolewa na bendi ya nyumba ya vipaji (THT), sambamba na wasanii kama Lina, Barnaba
na Wanne Star ambaye ni mwanamuziki wa muziki katika miondoko ya asili.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Mratibu wa shindano hilo William Malecela alisema
Redds Miss Ilala 2013 ataondoka na kitita cha sh. 1.5 huku mshindi wa pili
atapata zawadi y y ash. mil.1 huku
mshindi wa tatu atazawadiwa kiasi cha sh. 700,000.
Malecela
aliongeza kwa kusema kuwa mshindi wan ne atapata kitita cha sh. 400,000 na
watano atapata kiasi cha sh. 300,000 na watakaobaki watapata kifuta jasho cha
sh.200,000 kila mmoja.
Warembo
hao ni Natasha Mohamed (Ukonga), Irene
Mwelero (Mzizima), Diana Kato (Ukonga), Doris Mollel (Tabata), Anna Johnson(
Mzizima), Kazunde Kitereja (Tabata), Upendo Lema (Tabata), Alice Isack (Dar
City Centre), Matha Gewe (Ukonga), Kabula Kibogoti (Tabata), Rehema Mpanda
(Mzizima), Jenipher Kabunga (Tabata),
Clara Bayo (Dar City Centre) na Shamimu Mohamed (Mzizima), shindano hilo la
kumsaka Miss Ilala limepangwa kufanyika
Agosti 16 katika ukumbi wa Golden Jubilee Dar es Salaam.
0 Comments