TWANGA PEPETA WATAMBULISHA WANENGUAJI WAPYA

Baadhi ya wacheza shoo wapya wa Twanga Pepeta wakiwa jukwaani .
 
BENDI ya muziki wa dansi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’  jana  usiku ilitambulisha wacheza shoo wake wapya  katika onesho lao la usiku wa mwafrika lililorindima ndani ya ukumbi wa club bilicanas jijini Dar es Salaam.

Utambulisho huo ilifanyika  ikiwa ni baada ya wanenguaji hao kupatiwa mazoezi kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja ambapo sasa wataanza kuonekana katika jukwaa la Twanga Pepeta huku wanenguaji wakliotambulishwa ni Hamida Ibrahim , Samira Shaaban, Jamila Nassor, Stella George, Ester Fredy Hajra Abdallah  na Mwajuma Said ambao  licha ya kuwa ni wageni katika jjukwaa lakini walilitawala kwa muda  katika onyesho lililofanyika kwenye ukumbi wa Club Bilicanas.

 Aidha mbali ya kutambulishwa kwa madansa hao pia aliyekuwa mwanamuziki wa bendi hiyo wa siku nyingi Ige Moyaba ambaye anafanya kazi zake za muziki nchini Ubelgiji aliaga mashabiki wake na baada  ya kuja nchini kwa ajili ya kufanya  maonyesho manne  ambayo ni Idd Mosi, pili, katika Bonanza na Usiku wa Mwafika ambapo lilikuwa onyesho lake la mwisho huku akiahidi  kuja tena baadaye.

Moyaba atakumbukwa na mashabiki wa muziki jinsi alivyotamba katika kibao cha  Mtu Pesa na albamu hiyo kwa ujumla  iliyowapagawisha mashabiki na hata sasa bado iko katika chati kabla ya kuipa kisogo  bedni hiyo miaka 10 iliyopita.
 

Wakati huohuo wakiwa ndani ya Club Bilicanas Twanga Pepeta  walisindikiza utambulisho wa warembo wa takaoshindana leo katika shindano la urembo la Miss Ilala 2013 pichani juu.

Post a Comment

0 Comments