PRESS RELEASE
UTABIRI WA MWEZI APRILI VIONGOZI KUTEKWA NYARA
"Kuanzia tarehe 19 April na kuendelea hadi Julai mwaka huu, viongozi wa siasa na wafanya biashara maarufu wajichunge kutekwa nyara na kuibiwa, wao wenyewe na kufanywa kama bidhaa. Viongozi hao wachukue tahadhari nyakati zao za kutembea na wanaposafiri kwani pana uwezekano wasirudi, utekaji nyara huo ni wa viongozi tuliowataja na wasijiamini wanaposafiri au wakiwa kwenye mikutano wasiwe peke yao na wawe na mipangilio ya tahadhari nyakati zote. Nyota pia zinalenga wake na masahiba ya viongozi hao . Sheikh Yahya Hussein. Mnajimu Mkuu
Afrika Mashariki na Kati
P.O.BOX21250 DAR ES SALAAM
TEL+255754672464
Tukumbushane mapema mwezi Februari mwaka huu Sheikh Yahya alitabiri kutokea kwa vifo vya watu watu maarufu wasanii, na wanahabari ambavyo vingetikisa nchi ni kweli yalitokea kwa ajali iliyoua wasanii 13 wa kundi la Five Star na kifo cha mwanahabari wa siku nyingi Adam Lusekelo.
0 Comments