CHADEMA kimesema Jumamosi ijayo kitafanya maandamano nchi nzima kupinga muswada wa sheria wa mabadiliko ya Katiba unaoendelea kujadiliwa
Mbowe alisema lengo kubwa la maandamano hayo ni kupinga muswada huo kupelekwa haraka haraka na pia kukipa chama hicho fursa ya kupata maoni ya wananchi wengi zaidi.“Jumamosi wiki ijayo tunaandamana nchi nzima, wabunge wote wa CHADEMA watatawanyika nchi nzima, lengo ni kupata maoni ya wananchi wengi,” alisema Mbowe.
Alipinga hoja ya Serikali kwamba muswada huo usipopitishwa hivi sasa, hautakuwa na nafasi kwa sababu Bunge la Juni linahusika na Bajeti. Alisema miswada mingi imeshapitishwa kwa hati ya dharura
“Tunataka maoni ya wananchi wengi yakusanywe ili yazingatiwe, muswada uletwe bungeni Juni. Suala la kwamba Bunge la Juni ni la bajeti ni sawa, lakini mwaka jana uliletwa muswada wa Gharama za Uchaguzi kwa hati ya dharura ukapita,” alisema.
Mbowe alisema CHADEMA kitaendelea kupinga muswada huo kusukumwa haraka haraka na kuwakosesha wananchi fursa ya kuchangia na kwamba, iwapo makosa yatafanyika na kupitishwa hivi sasa, yatakuwa ni majuto makubwa siku zijazo.
wanaonyesha hisia zao,” alisema na kuongeza:
Muda wa ubabe kwa CCM umekwisha.“Waacheni wazomee, waacheni washangilie kama unawakataza kuzomea, wakati vijana wanaozomea kuhusishwa na CHADEMA Mbowe alisema kuzomea ni kuonyesha hisia na kwamba aze na kushangilia.
Mbona CCM wakishangiliwa hawakatai, sisi tunazomewa sana lakini tunaamini
“Kuna wanaozomea kama wabunge wa CCM humu ndani? (Bungeni), tunapoonyesha hisia zetu, hisia za wananchi kwa kutoka ndani ya ukumbi mnaona na kusikia jinsi wanavyotuzomea.”
Mbowe alisema kuzomewa kunawafundisha wanasiasa kusoma alama za nyakati na kwamba tuhuma za kila mara kwa chama hicho ni hofu ya watawala.Alisema suala la Katiba halitakiwi kubebwa na kuonekana kama ni mali ya kundi, chama au watu fulani, bali kushirikisha wananchi wote, huku akitahadharisha kuwa iwapo wataacha muswada huo kupita na upungufu huo, yatakuwa majuto makubwa siku zijazo.
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alidai muswada wa sheria unaopingwa na wadau takriban asilimia 90, hauwezi kusimamiwa kupita kwa nguvu ya dola.Kuhusu chama hicho kutuhumiwa kuhusika na vurugu, Mbowe alisema hizo ni propaganda kwa chama chochote cha siasa, lakini Chadema itaendelea kuhamasisha wananchi kudai haki zao. Chanzo http://www.uniquemodel/ blogspot.com
0 Comments