Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Stanslaus Nyongo, amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo, Richard Kayombo, kubaini na kuorodhesha wenyeviti wa vijiji na mitaa wanaochochea au kusababisha migogoro ya ardhi kwa makusudi ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Mhe. Nyongo ametoa agizo hilo leo Novemba 3, 2026, wakati akifungua kikao cha kupitia na kuhuisha Muongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Pwani kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kibaha.
Amesema baadhi ya viongozi wa maeneo wamekuwa wakihusishwa na vitendo vinavyochangia migogoro ya ardhi, hususan katika kipindi cha mauziano ya ardhi, hali inayoweza kuathiri mazingira ya uwekezaji. Ameelekeza viongozi watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuwa Serikali ya Mkoa wa Pwani ina mpango wa kuanzisha mfumo wa Duka la Ardhi utakaorahisisha upatikanaji wa huduma za ardhi na kuwawezesha wananchi kupata huduma za mauziano ya ardhi kwa utaratibu unaotambulika, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kupunguza migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani.
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani (RAS) Kayombo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Prof. Fortunata Makene, amesema kuwa mwongozo huo umeainisha fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Mkoa wa Pwani na ni nyenzo muhimu katika kuvutia uwekezaji, kukuza uchumi shirikishi na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Ameongeza kuwa mwongozo huo utasaidia kuitangaza Mkoa wa Pwani kwa wawekezaji na kutoa taarifa muhimu kuhusu fursa zilizopo katika sekta mbalimbali za kiuchumi.

0 Comments