Timu ya mpira wa wavu wanaume ya Jeshi la Magereza imeendeleza ushindani katika Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) 2026, baada ya kuibuka na ushindi wa seti 3–1 dhidi ya Timu ya JKT Tanzania, katika mchezo mkali uliofanyika leo Septemba 27, 2026 katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mchezo huo uliokuwa wa kusisimua na wenye mashambulizi makali kutoka pande zote mbili, uliwashuhudia wachezaji wa Magereza wakitumia vyema mipango ya ushambuliaji na kuweka ulinzi imara, hali iliyowawezesha kutawala mchezo na hatimaye kupata ushindi wa seti 3–1.
Ushindi huo umeongeza nguvu kwa timu hiyo katika mwendelezo wa mashindano hayo, huku Magereza ikiendelea kuonyesha ushindani mkubwa dhidi ya timu za majeshi na vyombo vya ulinzi na usalama vinavyoshiriki BAMMATA 2026.
Katika mchezo uliotangulia, Timu ya Kanda ya Magereza ilikutana na Timu ya Ngome ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambapo Magereza ilipata ushindi wa seti 3–2 katika mchezo uliokuwa wa ushindani mkubwa.
Matokeo hayo yanaendelea kuonyesha kiwango cha ushindani cha timu ya Magereza katika michuano hiyo, huku wachezaji wakiendelea kuweka nguvu na umakini katika michezo inayofuata.




0 Comments