WIZARA YA POKEA RUFAA YA MISS TANZANIA


WIZARA ya Habari , Vijana , Utamaduni na Michezo wamekiri kupokea rufaa kutoka  kwa  Kampuni ya Lino International Agency , ambao ndiyo waratibu wa shindano la Miss Tanzania.

Tanzania Daima ambayo ilifika katika Wizarani hapo  na kuzungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduni Lilly Beleko  alikiri kupoka rufaa hiyo.

“Nikweli Miss Tanzania wameleta barua yao ya kukata rufaa tumeiona lakini kama jinsi tulivyo serikalini jambo hili linakwenda ngazi kwa ngazi hivyo kuna utaratibu maalumu wa kutoa taarifa” alisema Beleko.

Mapema Januari  tano mwaka huu Kamati ya Miss Tanzania chini ya Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency , Hashim Lundenga walipelek barua ya kukata rufaa kuhusu shindano hilo kufungiwa kwa miaka miwili na Baraza la Sanaa la Taifa Basata na kuwataka wajipange upya.

Lundenga  alisema katika rufaa yao waliomba Wizara iwakutanishe wao na  Basata ili pande hizo mbili ziweze kujieleza huku akilalamika kwamba adhabu waliyopewa na Basata ni kubwa sana  ikilinganishwa na makosa  ambapo kosa kubwa ni kwa mawakala kuendesha shughuli  za kuandaa mashindano ya urembo bila ya kuwa na usajili kutoka Baraza hilo.
Basata walitangaza kulifungia shindano hilo la urembo kwa miaka miwili  Desemba 27  huku wakitoa  sababu mbalimbali ikiwemo mawakala wengi ambao huratibu shindano hilo katika ngazi mbalimbali kukosa sifa ya kutambuliwa na kusajiliwa na Basata

Post a Comment

0 Comments