BAGAMOYO SUGAR MABINGWA MKOA WA PWANI


 Timu ya Bagamoyo Sugar  ya Bagamoyo  wametwaa Ubingwa wa Mkoa wa Pwani RCL kwa 3-2 dhidi ya timu ya Kiduli yenye maskani yake Wilaya ya Kibaha. 

Akizungumza mara baada ya mechi hiyo iliyochezwa katika Uwanja wa Mwendapole Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani tarehe 12 Januari 2026 ,Mwenyekiti wa Chama Cha Mpira Wilaya ya Kibaha Kibafa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Pwani COREFA Robert Munisi amesema watatoa ushirikiano kwa timu hiyo.

" Tunawapongeza Bagamoyo Sugar kwa ushindi walioupata huku nawasisitiza wafuate utaratibu uliowekwa pia wakumbuke sasa hivi wao ndiyo mabalozi wa Mkoa wa Pwani kwa ujumla" amesema Munisi.

" Leo tumefikia tamati ya Ligi ya daraja la tatu Hivi sasa Bagamoyo Sugar hawapiganii Bagamoyo bali wanapigana kwa ajili ya Mkoa wa Pwani kwa ujumla natoa wito kwa wakaazi na wapenda mpira ndani ya Mkoa wa Pwani wote kwa pamoja tujipange katika kuhakikisha timu hii inaingia 'first eleven' tuzingatie kufanya usajili mzuri kwa kuzingatia umri wa U-20 tupate wawakilishi wazuri kwa ajili ya Mkoa" .


Aliyekua mgeni rasmi katika fainali hizo Rais wa timu ya Barberian ya Pwani Fidha  Helmis 'Tyson'  amesema kuwa amefurahishwa kutokana na kuona mchezo mzuri ameona vipaji kwa vijana wadogo U-20 ambao ni fahari kwa Mkoa wa Pwani.

Aidha Mwenyekiti wa timu ya Bagamoyo Sugar Kelvin Mawata amesema kuwa timu hiyo inahudumiwa na Kiwanda na kukiri kuwa licha ya kuzalisha sukari wameunda timu yao ambayo wanaihudumia kwa kila kitu.

"Tunaomba wadau wa michezo pamoja na mashabiki watupokee na tumeikabidhi timu kwa wananchi tutapokea maoni na changamoto zote illi tuweze kufika mbali" amesema Maweta.

Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Wilaya ya Bagamoyo Salum Kanema amesema Viongozi wamefarijika na kuandika historia ya soka ndani ya Mkoa wa Pwani.
" Nawapongeza Bagamoyo Sugar kwa ushindi huu wametujengea heshima na kuweka alama kwa sisi Viongozi wasiishie hapa twende tukapande na kucheza Ligi Daraja la Pili" amesema. 

Post a Comment

0 Comments