Na Mwandishi wetu, Dodoma.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeshiriki mkutano mkuu wa Chama cha Mahakimu na Majaji Tanzania kwa lengo la kunadi vivutio vya utalii na kuimarisha ushirikiano kati ya Ngorongoro na Mahakama.
Mkutano huo uliofunguliwa tarehe 13 januari, 2026 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan unaendelea hadi tarehe 16 Januari, 2026 ambapo wadau mbalimbali wa sekta ya sheria kutoka maeneo tofauti ya nchi wanashiriki kujadili masuala mbalimbali yanayohusu haki, utawala wa sheria na maendeleo ya mfumo wa utoaji haki nchini.
Ujumbe wa Ngorongoro uliongozwa na Kamishna msaidizi mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia idara ya utalii na Masoko Mariam Kobelo pamoja na Afisa Uhifadhi mwandamizi-Sheria Usaje Mwambene ambapo mada mbalimbali kuhusu vivutio vya utalii, fursa za uwekezaji, huduma zinazotolewa na upekee wa Ngorongoro kama kivutio bora cha utalii barani afrika kwa mwaka 2023 na 2025.Aidha, NCAA imetumia mkutano huo kujenga uelewa kwa wadau wa sheria kuhusu misingi ya kisheria inayosimamia uhifadhi wa rasilimali za asili ili kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ikiwemo Kreta za Ngorongoro, Empakai, Olmoti, maporomoko yaa maji endoro, Ndutu ambalo ni maarufu kwa mazalia ya nyumbu wanaaohama, mchanga unaohama, makumbusho ya olduvai, makumbusho na jiopaki na vingine vingi.





0 Comments