MSHINDI wa
shindano la Big Brother Africa Hot Shots ,Idriss Sultan amewataka wasanii kutokubali kutumika na badala yake wajitambue ili kulinda hadhi
yao.
Idrissaliyasema
hayo jana Jijini Dar es Salaam ambapo pia amewataka wasanii wa hapa nchini
wajenge tabia ya kuwa na mikataba katika kazi wanazozifanya ili kuweza kulinda
maslahi yao ya kazi kwa ujumla.
“Wasanii wengi hapa nchini hawana ufahamu juu ya umuhimu wa utaratibu wa kusainisha mikataba mapromota
ambao wakati mwingine huwaacha kwenye mataa na kuwaacha wakibwabwaja” alisema
Sultan.
Kwa mujibu
wa Sultan pia ametia msisitizo wasanii hao wawe na Mawakili ambao watakuwa
wakiwasaidia katika kazi zao.
Hadi hivi
sasa ni wasanii wawili tu ambao ndiyo wenye mikataba na mawakili ambao ni
Ambwene Yesaya ‘AY’ na Khamis Mwinjuma ‘MwanaFA’.
0 Comments