BARBERIAN WAWACHEZESHA KWATA 2-1 TMA


Timu ya Soka Mkoa wa Pwani Barberian jana tarehe 11 Januari 2026  jioni wamewachezesha kwata Maafande wa timu ya  TMA  yenye maskani yake Jijini Arusha 2-1 katika mechi ya Ligi Daraja la Kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Filbert Bayi Mkuza Kibaha.

Awali TMA walitikisa nyavu za wenyeji wao Barberian ambao walisawazisha hadi mwisho wa mchezo Barberian wametoka kifua mbele kwa kuongoza na kujipatia Pointi tatu. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya mchezo kumalizika Kassim Salehe Haruna amesema wamefurahishwa na matokeo hayo.

"Matokeo haya ni kwa sababu tumesikiliza nakutekeleza maelekezo ya Mwalimu wetu na tuliamini kuwa tutaweza licha ya kuwa wenzetu walitutangulia kwa kutufunga tulifanya mabadiliko katika uchezaji," amesema Kapteni wa Barberian Kassim.

Kocha wa Barberian Julio Elieza amesema kuwa matokeo ya mechi hiyo yametokana jinsi walivyojipanga na kutambua uchezaji wa wapinzani wao TMA mpango wa mechi hii 
umekwisha sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi ijayo .

Wakati huohuo Kapteni wa Timu ya TMA yenye  maaskani yake Jini Arusha  Fadhili Mahimbo amesema kuwa licha ya timu yake kuanza kufunga goli changamoto imekuwa miongoni mwao kwani wamecheza vibaya .

"Changamoto ni sisi wachezaji tumecheza vibaya ila naahidi katika mchezo ujao tutacheza vizuri na timu ya Gunners ya Njombe tunakwenda kufanyia kazi makosa yote yaliyojitokeza ili tuweze kufanya vizuri na kusonga mbele,"amesema Kapteni wa timu ya TMA Fadhili.

"Sisi wenyewe tumecheza bila kuelewana na kutofuata alichokitaka Kocha tuna imani Waalimu wameangalia mchezo wameng'amua wapi kwenye upungufu," amesema Fadhili.

Naye Mwalimu wa Timu ya TMA Tiko Tiko amesema kuwa mchezo umeanza huku wachezaji wake wakiwa chini sana katika kipindi cha kwanza pia wamebakiza mechi tano ambazo zote watacheza ugenini.

"Katika mechi za ugenini kuna changamoto ya ugeni tunakwenda kufanyia kazi kwa sababu huwa kuna 'Game Plan' ya wenyeji.

Post a Comment

0 Comments