MWADHAMA POLYCARP KARDINALI PENGO ANAKABILIWA NA CHANGAMOTO ZA KIAFYA ATAKWENDA INDIA KWA MATIBABU

Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Juda Thaddeus Ruwa’ichi, amesema hali ya afya ya Kardinali Policarp Pengo, siyo nzuri kutokana na changamoto za kiafya zinazomkabili.

Taarifa ya Askofu Ruwa’ichi imetolewa leo tarehe 24 Desemba  2025  imetoa wito kwa Wakatoliki kumwombea Kardinali Pengo.

“ Mzee wetu mpendwa Kardinali Policarp Pengo anakabiliwa na changamoto za kiafya. Zimefanyika jitihada za kumsaidia kimatibabu hapa kwetu. Hata hivyo, imeonekana kwamba upo uhitaji wa kumpeleka nje  ya nchi ili apate matibabu ya uhakika zaidi.

“Kwa hiyo, mipango imefanyika ili akatibiwe mchini  India. Tunatarajia kwamba ataondoka hivi karibuni  kwa lengo la  kupata matibabu hayo. Ninawaalika nyote tuungane kumsindikiza kwa sala na matashi mema,” amesema Askofu Ruwa'ichi


 

Post a Comment

0 Comments