Mazishi ya mwanamuziki Faliala Mbutu ambaye alikua mume wa mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Luiza Mbutu yatafanyika Jumatatu tarehe Desemba 29 ,2025 maziko yatafanyika katika makaburi ya Kwa Kondo, Bahari Beach Jijini Dar es Salaam.
Wakati huohuo mwanamuziki mkongwe wa bendi ya The African. Stars ' Twanga Pepeta' Jojoo Jumanne ametoa maelekezo namna ya kufika msibani amesema ukishachukua barabara ya Salasala kutoka kituo cha Mbuyuni, unakwenda hadi mwisho wa lami kisha unauliza kwa Mama Neema Mganga ambaye ni maarufu sana hapo mwisho wa lami.
"Ukifika hapo kwa Mama Neema tayari utaiona nyumba ya msiba." amesema Jojoo.
Marehemu Faliala Mbutu alikuwa mtoto wa mwanamuziki wa zamani wa Orchestra Makakassy .

0 Comments