Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) katika utekelezaji wa majukumu kisheria imebaini kuwa kuna baadhi ya watu wasio na sifa wamerejea kutekeleza majukumu ya kihabari baada ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu.Katika muktadha huo Bodi inakumbusha na kusisitiza kuwa Uandishi wa habari ni taaluma rasmi iliyorasimishwa kwa misingi ya kisheria ,maadili na weledi wa kitaaluma na hivyo mtu yeyote anayejuhusisha na shughuli za kihabari bila kuwa na Ithibati anakiuka masharti ya kifungu cha 19 cha Sheria ya Huduma za Habari sura 229 Toleo la 2023.
Aidha kwa mujibu wa kanuni ya 17 (1)(a) ya kuhusu sheria ya Huduma za Habari, Tangazo la Serikali Na.18 la Tarehe 2 Februari ,2017 wanaopaswa kuwa na Ithibati ni pamoja na Wahariri, Waandishi wa Habari, Waandishi Huru (Freelancers) ,
Wapiga Picha ,Wazalishaji wa vipindi na Watangazaji wa Redio na Televisheni wanaofanya kazi katika vyombo vya habari.
Kwa muktadha huo Bodi inatoa ONYO na kuwataka watu wote wanaofanya kazi za kihabari bila kuwa na Ithibati kuacha maramoja kwani kuendelea kufanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 50 (2)(b) cha Sheria ya Huduma za Habari Sura ya 229 .Aidha haitasita kuchukua hatua stahiki za Kisheria dhidi ya mtu au taasisi yoyote itakayobainika kuajiri au kuruhusu utekelezaji wa shughuli za kihabari bila kuzingatia utaratibu na masharti yaliyowekwa kwa mujibu wa Sheria.
Vilevile, Bodi inautaarifu umma na wadau wote wa sekta ya habari kuwa katika kipindi cha hivi karibuni itaendesha ukaguzi maalum katika vyombo vya habari na maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kujiridhisha kuwa watu wote wanatekeleza wanakidhi vingezo kwa mujibu wa Sheria. Ikumbukwe kuwa utoaji wa Ithibati kwa Waandishi wa Habari ni kuongeza uaminifu wa taarifa zinazozalishwa na kusambazwa
kuwapatia Waandishi ulinzi wa Kisheria wanapotekeleza majukumu ya kihabari wanakidhi vigezo vikivyoainishwa kwa mujibu wa Sheria.
Ikumbukwe kuwa ,utoaji wa Ithibati kwa Waandishi wa Habari si kikwazo cha huru wa habari bali ni nyenzo muhimu ya kulinda heshima na hadhi ya taaluma ya uandishi wa habari, kuongeza uaminifu wa taarifa zinazo zalishwa kusambazwa kwa umma pamoja na kuwapatia Waandishi ulinzi ulinzi wa Kisheria wanapotekeleza majukumu yao.
Bodi inatoa wito kwa watu wote wenye nia ya kufanya kazi za kihabari kuhakikisha wanapata Ithibati kwa mujibu wa Sheria,
wana zingatia maadili na weledi wa juu wa taaluma na kutumia kalamu ,sauti na majukwaa yao kwa kuwahudumia wananchi kwa kutoa taarifa sahihi,kukuza uwajibikaji na kuchangia maendeleo endelwvu ya Taifa.
Imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) Patrick Kipangula.


0 Comments