ACT WAZALENDO WAITWA KUUNDA SERIKALI ZANZIBAR




 Na Mwandishi Wetu, Zanzibar


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kina imani na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) kwani ndio mfumo ambao waZanzibari waliuchagua.

Akizungumza Ofisini kwake, Kisiwandui Unguja. Katibu wa Kamati Maalum NEC Zanzibar Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema njia ya kutatua changamoto za waZanzibari ni kufanyakazi pamoja.

Kulingana na Katiba ya Zanzibar, chama kinachoshika nafasi ya pili kwa wingi wa kura hutoa Makamu wa Kwanza wa Rais na wingi wa viti vya Uwakilishi chama hicho hupata nafasi za Uwaziri na mchakato huo unatakiwa ukamilishwe ndani ya siku tisini.

Alisema kutokana na ACT Wazalendo kupata viti 10 vya Uwakilishi katika Uchaguzi Mkuu uliopita 29 Oktoba 2025, inapata nafasi 4 za uWaziri lakini hadi sasa vipo wazi wakati shughuli za serikali zinaendelea.

"Ukisema uhusiki maana yake nini? Unalalamika, rudi uwatumikie wananchi hadi hukumu itakapotoka" alisema Mbeto.

Alisema busara itumike kwa kuwatumikia wananchi wakati unaendelea na malamiko kwenye mfumo wa mahakama walipoenda kwani wakishinda viti vya uwaziri vinaongezeka.

"Tunataka waje, tuunde serikali ya pamoja na huo ndio msimamo wa CCM" alisema Mwenezi Mbeto na kuongeza kuwa ingawa yeye si msemaji wa serikali lakini iliyopo madarakani ni ya CCM hivyo chama hicho serikali inayotaka ni ya Umoja wa Kitaifa.

Post a Comment

0 Comments