Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Mawazo Nicas (mwenye suti) ametoa amri ya kufungwa kwa Viwanda viwili kwa kosa la kutiririsha maji taka yenye sumu na kinyesi yanayo athiri wananchi katika eneo hilo.
Viwanda vilivyofungiwa ni Radiant kinachotengeneza vinywaji na vipodozi na Kiwanda cha Fortune Paper Group Limited vyote vipi katika Kata ya Misugusugu Manispaa ya Kibaha Wilaya ya Mkoani Pwani.
"Nimefikia uamuzi wa kuvifungia Viwanda hivi baada ya kupokea malalamiko kwa wananchi kwamba wanatiririsha maji machafu yanayotoka Kiwandani pamoja na maji ya machafu ya chooni jambo linalopelekea kuathiri afya za wananchi wanaoishi katika eneo husika" amesema Dkt. Nicas.
Hatua ya kukifungia Kiwanda hicho imechukuliwa jana tarehe 31 Desemba 2025 ambapo wananchi wametoa kero hiyo kwenye mkutana wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Shule ya Miomboni Kata ya Misugusugu Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.
Wanananchi hao wametoa malalamiko ba kusema kuwa maji hayo yanayotiririshwa kutoka Kiwanda hichi cha Radiant yanaathiri afya zao huku baadhi wakionesha kupasuka nyayo na kuvimba miguu nyayo miguu baada ya kukanyaga maji hayo ambayo pia imedaiwa yanakausha mazao yanayolimwa na wananchi kwenye eneo husika wakitaja baadhi ya mazao ni mahindi mbogamboga za majani na matango.
Dkt. Nicas baada ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi aliamuru jopo la wataalam kwenda kuona hali galisi katika eneo linalolalamikiwa na wananchi na mara baada ya kuona ndipo Mtaalamu pamoja na Afisa Mazingira na wengineo walipofika wakashuhudia maji machafu na yenye harufu kali yakitiririka kutokakiwandani.
Dkt. Nicas ameshuhudia ujenzi holela wa mfereji unaolalamilkwa unaotiririsha maji hayo machafu na kuathiri afya za wananchi ndipo akaamuru Kiwanda kifungwe hadi watakapotekeleza kwa kufuatiamiongozo ya mazingira.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Mrisho Mlela amekiri kwa kusema hali ambayo wameishuhudia siyo rafiki kwa wanachi na amesisitiza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Radiant afuate maelekezo ambayo amepewa mara kadhaa na Baraza la Uhifadhi wa Mazingira NEMC ,inasikitisha sana kuona Kiwanda kimepewa maonyo mara tatu lakini hakuna utekelezaji.
"Wameonywa mara tatu na yeye Mahesh anakubali hilo lakini bado tu hakuna utekelezaji wa aina yoyote malalamiko ya wananchi yamekua mengi ,hivyo wanahitaji na sisi Viongozi tuje hapa kulalamika hii haiwezekaniamesema Mh.Meya Dkt. Nicas.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha Mrisho Mlela ameongeza kwa kusema kuwa "kwakuwa hawajatii sheria za usimamizi wa mazingira hivyo tunasimamisha shughuli za uzalishaji hadi pale watakapo tekeleza ujenzi wa mabwawa ya maji taka kama walivyoelekeza ambayo hayaleta madhara kwa wananchi ".
Baraza la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC )kwa kushirikiana na Maofisa
Mazingira wa Manispaa ya Kibaha wamefika kwenye viwanda hivyo na kutatua kutoa ufumbuzi wa haraka wa kudhibiti uchafuzi huo wa mazingira.
Ofisa Mazingira Manispaa ya Kibaha Raheli Ulaya amekiri kutoa onyo zaidi ya tatu lakini wamiliki hao hawajaonesha kutii hivyo amevifungia kwa muda hadi hapo hali itakaporidhisha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kutolewa amri hiyo Mkurugenzi wa Kiwanda Cha Radiant amejitambulisha kwa jina moja tu la Mahesh huku akigoma kutaja jina lake la pili amesema hakuna lazima amekiri udhaifu huo na kweli amepewa onyo mara tatu na hakuna walichotekeleza hivyo ameahidi ndani muda wa miezi mitatu watajenga na kurekebisha mifumo ya maji taka pamoja na mabwawa ya kutiririsha majitaka kutoka kwenye cha Radiant kwa kufuata
taratibu na Sheria za Mazingira kwa kuweka mifumo ya kisasa ya kuchuja maji taka na zenye kemikali .

















0 Comments