USIKU WA LUIZER MBUTU SASA KURINDIMA JANUARI 7

BENDI ya The African Stars 'Twanga Pepeta' kwa mara nyingine tena imesogeza mbele onyesho la Usiku wa Luiza Mbutu onyesho ambalo lilikuwa lifanyike Januari 31 mwaka huu sasa litafanyika Februari 7 kwenye ukumbi wa Mango Garden Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Usiku wa  ‘Luizer Mbutu’ ni onyesho ambalo linalenga kumuenzi mwanamuziki huyo wa kike ambaye  ameonyesha msimamamo wa kukaa katika bendi hiyo kwa muda wa miaka 16 sasa bila kuhama kama jinsi ilivyo kwa wanamuziki wengine.
 Mbali ya usiku huo ambao bendi ya Twanga Pepeta itakuwa ikitimiza mika 16 tangu ilipoasisiwa  hivyo kwa sherehe za mwaka huu uongozi umeamua kumtunuku Luizer na kuuandaa maalum kwa ajili yake.
Awali onyesho hilo lilikuwa lifanyike Desemba 20 mwaka jana likaahirishwa hadi Januari 31 kutoka na msiba wa  mnenguaji Aisha Madinda ambaye alipanga kushiriki lakini bahati mbaya akawa amefariki dunia.
Kiongozi wa bendi hiyo Luizer  Mbutu alisema  onyesho hilo limeahirishwa kwa mara ya pili kutokana na maombi ya
baadhi ya mashabiki ambao wanatarajia kushiriki.
"Tumeona ipo haja ya kuwasikiliza na sasa onyesho litafanyika Februari7 "alisema Mbutu.
Alisema kuwa wamealikwa wanawake wa fani mbalimbali ili waje wamshuhudie mwanamke mwenzao kile ambacho amewaandalia katika onyesho hilo ambalo limepewa jina la 'Usiku wa Luizer Mbutu'.
Wasanii mbalimbali watapamba usiku huo ambao ni Kiongozi wa bendi ya UtaliiSound, Hamza Kalala 'Mzee wa Madongo',
Stara Thomas, Sizza Mazongera 'Mamaa wa
Segere', Bob Gaddy, Banza Stone, Adolph Mbinga na wengineo wengi
watakuwepo," alisema.

Post a Comment

0 Comments