ARUBAINI YA MAREHEMU AISHA MADINDA JUMAPILI JANUARI 25

KISOMO cha kumrehemu marehemu Aisha Madinda kimepangwa kufanyika Jumapili Januari 25 nyumbani kwao Mikadi Beach Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamethibitishwa na Mkurugenzi wa ASET , Asha Baraka ambaye alikuwa bosi wa marehemu katika enzi za uhai wa Aisha Madinda.
Asha amewaomba wadau , ndugu jamaa na marafiki kujitokeza kwa wingi siku hiyo ikiwa ni katika kumuenzi pia.
Marehemu Aisha alifariki siku  tatu kabla ya kutambulishwa upya katika jukwaa la Twanga Pepeta ambako alikuwa amepanga kurudi baada ya kuipa kisogo bendi hiyo kwa miaka kadhaa.
Aisha alivuma sana katika safu ya unenguaji na kujizolea mashabiki lukuki  pamoja na wadau mbalimbali wa muziki  kama Zahir Ally Zorro, Ally Choki na wengine mbalimbali  wakisema kwamba hajawahi kutokea mnenguaji mahiri nchini kama jinsi alivyokuwa msanii huyo.

Marehemu Aisha alizikwa katika shamba lao lililopo Mikwambe Kigamboni.

Post a Comment

0 Comments