KUNDI la muziki wa taarabu la Ogopa Kopa limeongezwa katika
orodha ya bendi zitakazotoa burudani katika tamasha la muziki la CDS
linalotarajiwa kufanyika viwanja vya TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam
Januari 25.
Akizungumzia tamasha hilo, Mratibu Hamis Dakota pichani juu , alisema wameamua kuliongeza
kundi hilo ili kuongeza ladha.
Dakota alizitaja bendi nyingine zitakazotoa burudani siku
hiyo kuwa ni FM Academia, Malaika Band, Mapacha Watatu na wakongwe, Msondo
Ngoma ‘Baba ya Muziki’.
Tamasha hilo linadhaminiwa na CDS, Global Publishers na
Clouds FM, ambako limepangwa kuanza saa 12 jioni kwa kiingilio cha sh. 5,000.
0 Comments