NAIBU WAZIRI
wa Wizara ya Fedha Mwigulu Nchemba Pichani juu amesema kwamba katika nchi ya Tanzania
mchakato wa kupata vazi la taifa utakuwa mgumu kutokana na wingi wa makabila.
“Unajua
Tanzania ni nchi kubwa hivyo kutokana na
wingi wa makabila yaliyomo ndani yake ni vigumu kupata vazi moja ambalo
litakubalika na kila kabila huku akiwataja, wamasai, wasukuma na wengineo hivyo ndiyo sababu akaamua yeye
binafsi kubuni kuvaa skafu ambayo ina rangi za bendera ya nchi”alisema
Nchemba.
Aliendelea
kwa kusema kuwa yeye hupendelea kuvaa skafu yenye kufumwa na nyuzi za sweta
kutokana na kupata msukumo kutoka kwa na baadhi ya viongozi kuwa na mitindo ambayo iliweza kuwatambulisha katika jamii.
“Kutokana na
hilo nami nikapatwa na mguso wa kuwa navaa skafu yenye rangi za bendera ya
taifa ikiwa ni njia moja wapo ya kujitambulisha vilevile skafu ni vazi jepesi ambali linaweza kuvaliwa na mtu yeyote" anasema.
0 Comments