DC KIBAHA : MADIWANI CHALINZE ,KIBAHA NENDENI MKASIMAMIE MIRADI



Madiwani Kibaha na Chalinze Watakiwa Kuwa Mabalozi wa Usimamizi Bora wa Miradi ya Maendeleo 

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon, amefungua mafunzo elekezi kwa madiwani wa Halmashauri za Wilaya ya Kibaha na Chalinze yaliyofanyika leo Januari 15, 2026, katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

hayo, Mhe. Nickson amewataka madiwani kuwa mabalozi wazuri wa usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata zao, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji na ufuatiliaji wa karibu wa miradi hiyo. Amebainisha kuwa amekuwa na desturi ya kutoa zawadi kwa madiwani wanaofanya vizuri katika kusimamia miradi ya maendeleo.

“Madiwani mnapaswa kuwa wakali katika kufuatilia utekelezaji wa miradi na sheria za Halmashauri kwa kutumia takwimu sahihi, lakini msijenge ukali kwa watu au kushughulikia masuala binafsi,” amesema Mhe. Nickson.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo 

Aidha, amewasisitiza madiwani kutumia lugha ya staha wanapotekeleza majukumu yao ya uongozi, akieleza kuwa lugha ya kiongozi ni msingi wa mahusiano mazuri kati ya viongozi, wataalam na wananchi.

“Chuki na hasira zisihitimishe mazungumzo yenu na Wakurugenzi pamoja na wataalam. Kosoeni miradi, siyo watu,” amesisitiza.

Katika mafunzo hayo, Mhe. Nickson amewahimiza madiwani kujifunza kujishusha na kujipandisha kulingana na mazingira ya uongozi, akibainisha kuwa kiongozi bora anatambua wakati wa kuwa kiongozi na wakati wa kuwa raia wa kawaida. Pia amewataka kujiepusha na tamaa ya kujinufaisha na mali za umma, kukubali kukosoa na kukosolewa, na kufanya kazi kwa ushirikiano bila ubaguzi wa kisiasa.

Post a Comment

0 Comments