HUSNA ABDUL 'DAHU' akizungumza na waandishi wa habari nje ya Wodi ya watoto katika hospitali ya Amana ambako alizaliwa miaka kadhaa iliyopita.
MSANII Zuwena Muhammed (Shilole), jana alikuwa kivutio tosha katika
wodi ya watoto wachanga katika hospitali ya Amana Jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Shilole
aligeuka kuwa kivutio baada ya kuwa akiitwa na kina mama waliojifungua na
kutaka abebe watoto wao na kupiga nao picha.
Aidha msanii
huyo alifika hospitalini hapo akiwa ameambatana na msafara wa Balozi wa watoto wa
kuanzia umri wa kuzaliwa hadi miaka mitano Husna Abdul ‘Dahu’ ambaye ni
mtangazaji wa kituo cha Clouds FM aliyekuwa akiadhimisha siku yake ya kuzaliwa
kwa kutoa zawadi kwa watoto wachanga na vifaa tiba kwa hospitali katika kitengo
hicho.
Aidha
Shilole ametangaza rasmi kumuunga mkono Dahu katika kazi zake za kijamii ambapo
atakuwa msanii wa kwanza kumuunga mkono
katika kila hatua ya ubalozi wake kwa watoto hao hospitalini hapo.
“Hili ni fundisho tosha kwa wasanii na hata
watu wengine katika jamii tubadilike sasa tuwe tunaadhimisha siku kwa namna ya
kufanya mrejesho katika jamii kama alivyofanya Dahu amenigusa sana na mimi
nitafanya hivyo nitakwenda Igunga siku yangu ikifika” alisema Shilole.
Aidha
shilole aliweza kubeba watoto kadhaa katika wodi hiyo ya watoto na akampa mtoto
mmoja jina lake la ‘Shishi Baby’ huku akimsisitiza mama wa binti huyo mchanga
ampe na aitunze picha waliyopiga sambamba na la ‘ShishiBaby’.
“Nilizaliwa
tarehe 25 Januari 1986 katika hospitali hii ya Amana hivyo nimeona leo ikiwa ni siku yangu ya kuzaliwa
nije kushereheka kwa namna nyingine
kabisa kuwaona watoto wachanga ambao wamezaliwa tarehe kama yangu na
kuwapa zawadi wazazi na kutoa msaada wa
vifa tiba” alisema Dahu.
Dahu
alizungumza hayo leo wakati akikabidhi vifaa hivyo vyenye
thamani yash. Mil.1 ambavyo pia vimetolewa kwa msaada wa kituo cha Clouds FM.
Muuguzi wa
wodi hiyo ambaye Mwanaidi Msai alisema watoto waliozaliwa ni 37
huku 20 wakike na 17 wa kiume .
Pia wamemshukuru Dahu kwa kujitoa na
kuwaomba wasanii wengine waliozaliwa katika hospitali hiyo akiwemo Naseeb Abdul
‘Diamond Platinumz’ na viongozi
mbalimbali waliozaliwa katika hospitali ya Amana wafike kuwasalimia katika hospitali waliyozaliwa.
Dahu akikabidhi vifaa hivyo leo.
0 Comments