Wizara ya Afya imeanza kambi maalum ya siku 30 ya upasuaji na uchunguzi wa magonjwa ya mabusha na matende kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kambi hiyo ilianza Januari 5, 2026 na tayari watu 127 kati ya165 waliojitokeza kufanyiwa uchunguzi wa awali wamebainika kuwa na viashiria na dalili za ugonjwa wa mabusha katika mkoani Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa leo Januari 8,2026 na Mganga Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Dk.Mohamed Mang'una katika mkutano wa vyombo vya habari uliondaliwa na Wizara ya Afya Mpango wa Kuzuia Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele.
Dk.Mang'una amesema watu hao wamebainika katika kambi Maalum ya zilizopo Kituo cha Afya Kilakala Temeke na Kituo cha Afya Kinondoni.
Amesema kati ya hao 127 waliobainika katika kambi hizo 67 tayari wako wodini kwaajili ya kuwaandaa kupasuliwa katika vituo maalum vilivyoandaliwa na Wizara ya Afya huku wakiendelea kuchunguza wengine wanaojitokeza katika vituo hivyo.
Aidha amefafanua ugonjwa huo unatokana na sababu tofauti vinavyotokana na vimelea ikiwemo minyoo , mbu na wagonjwa wengi wanaokumbwa na shida hizo ni wale waishio mikoa ya Pwani ikiwemo Mtwara,Lindi,Tanga, Dar es Salam na kwingineko.
Magonjwa hayo yasiyoambukizwa na yasiyopewa kipaumbele nchini watanzania wametakiwa wasiyadharau kwakuwa yanawapata watu wa kada zote wakowemo vijana, wazee na hata wanawake hivyo watu wote wanatakiwa wajitokeze kuangalia afya zao.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Saad Mtambule akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amesema wananchi wanatakiwa wajitokeze kupima afya zao katika kambi hizo na wataweza kupatiwa matibabu bure Serikaki itagharamia kwa asilimia 100.
"Kati ya uwekezaji mkubwa unaofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anataka ahakikishe magonjwa haya yasiyoambukiza yanatokomea na kuisha kabisa Tanzania hivyo jitokezeni mje mfanyiwe uchunguzi na mtibiwe Serikali iko pamoja na wanachi wake" amesema Mtambule.
Amesema katika kampeni ya hiyo Serikali imeadhimia kufikia watu zaidi ya 1000 ndani ya Mkoa wa Dar Salaam
WAKAZI WA DAR ES SALAAM WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA UPASUAJI WA MABUSHA BURE


0 Comments