IKIWAni siku
chache tu kupita tangu Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo Ally Choki (Wazee wa Kizigo) pichani kulia kupanda katika
jukwaa la bendi ya Twanga Pepeta
Jumapili iliyopita katika bonanza linalofanyika kwenye viwanja
vya Leaders Club mashabiki wamponda huku wengine wakisifia kitendo hicho.Wapo waliosema kwamba Choki amesambaza upendo kwa mwana mama Asha Baraka lakini wengine Asha mwenyewe amejibu mapigo na kusema hajastushwa na kitendo hicho kwa ilivyo kwa wengine.
Akizungumzia jambo hilo Mkurugenzi wa bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka alisema kwamba hajashangazwa na tukio hilo kwani anajua wasanii hupanda kwenye majukwaa ya bendi nyingine ikiwa ni namna ya kusalimiana.
“Alipopanda jukwaani mimi sikuwepo nilikwishaondoka hivyo hiyo sehemu ya wasanii kusalimiana wenyewe kwa wenyewe , lakini pia napenda kuwaambia wasanii wawewanaweka maneno akiba kwani katika maisha kuna leo na kesho" anasema Asha.
Aisha anaendelea kwa kusema kuwa "nasema hivyo kwa sababu siku zote Choki yeye ndiye anaye zungumza hivyo mimi sitaki kuzungumza lolote zaidi ya kutolea mfano kwamba hata Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ anapaswa akumbuke walikomtoa kina Ruge Mutahaba na siku zote hakuna mabaya yanayoendelea na mtu akikukosea bora kumwita pembeni na kumweleza siyo kwenda kwenye vyombo vya habari na kuzungumza” alisema Asha.
Choki
alifika katika viwanja vya Leaders Club mapema jioni siku ile ambapo wasanii wa
bendi ya Twanga walisikika wakisema kaka Ally kaja hivyo wakawa wakienda
kumsalimia kila mmoja kwa wakati wake.
Baadaye
ndipo Choki alipopanda kwenye jukwaa na kuimba wimbo wa ‘Password’ ambao ni
utunzi wake Choki albamu aliyoitunga kabla
hajaipa kisogo bendi hiyo.
Wakati
huohuo Choki alitafutwa kwa njia ya simu simu yake ilikuwa imezimwa.
0 Comments