MASHABIKI waliohudhuria burudani katika kituo cha maraha cha Dar Live huko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam walipata starehe ya kutosha kutoka kwa wanamuziki Juma Kassim ‘Sir Nature’ wa hapa nchini, na Namelesa kutoka Kenya ambapo walitoa makamuzi ya nguvu usiku wa kuamkia leo.
Wanamuziki hao walitoa kauli za kuushukuru umati mkubwa uliojitokeza kwenye onyesho hilo wakisema hawakutegemea Mbagala kuwa na mashabiki wa burudani wengi hivyo.
Shoo hiyo ilisindikizwa na Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Mashauzi Classic Band, Wakali Dancers, Zuhura na wasanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya huku washiriki wa shindano la “Cheza, Vaa Imba Kama Rihanna” wakitambulishwa kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo.
Mwanamuziki Ambwene Yesayah ‘AY’, akiwasalimia mashabiki.Akiwajibika jukwaani.
Juma Nature “akipeana tano” na mashabiki wake kabla ya makamuzi.
Kundi zima la Wanaume Halisi likiwajibika jukwaani.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Zuhura, akipagawisha mashabiki.
Isha akiwa kazini.
.
Mshiriki wa shindano la “Cheza, Vaa, Imba Lama Rihanna” akionyesha uwezo wake wakati wa utambulisho wao.
“Rihanna” mwingine akionyesha uwezo wake.
Wasanii wa kundi la Wakali Dancers wakikamua wimbo wa Michael Jackson.
Wanenguaji wa FM Academia wakionyesha uwezo wa nyonga zao..
Kina “Rihanna” wakionyesha ujuzi wao.
Juma Nature akiongea na mashabiki wake.
Wanamuziki wa bendi ya FM Academia wakiwajibika jukwaani.
: Mashabiki waliofurika katika tamasha hilo wakifuatilia burudani hiyo.
Hali halisi ya umati ulioingia ukumbini hapo
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL
0 Comments