BAADA YA KUSIMAMIA BENDI SASA ASHA BARAKA KUSAKA VIPAJI VYA WAPIGA ALA ZA MUZIKI

 MKURUGENZI wa Kampuni ya The African Stars Entertainment ASET, Asha Baraka ametangaza kutoka kivingine kwa kuanzisha Taasisi ya kuvumbua vipaji itakayokwenda kwa jina la Twanga Academia.

Akizungumza jana na waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika Katika ukumbi wa Mango Garden Dar es Salaam  leo kwamba Twanga Academia wamenunua vifaa vyenye thamani ya sh. Mil 100 kwa kuanzia.
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa katika taasisi hiyo wamepanga kufanya usaili umepangwa kufanyika Jumapili ijayo katika viwanja vya Leaders Club, Februari 12 ambapo usaili huo utaanza saa sita mchana.

Baraka aliongeza kwa kusema kuwa katika usaili huo utasimamiwa na magwiji wa muziki wa dansi ambao pia ni wanamuziki kama Hamza Kalala ‘ Mzee wa Madongo’ na wengineo kadhaa ambapo watatoa fursa kwa chipukizi wanye uwezo wakutumia ala za muziki.

Aidha Asha anawataja baadhi ya walimu wa Twanga Academia watakuwa Rais wa bendi ya FM Academia Nyoshi El Saadat,

“Lengo la Twanga Academia ni kusaka vipaji vya waimbaji pamoja na wanamuziki wenye uwezo wa kupiga ala ambavyo vitaendelezwa kwa kupitia wakufunzi watakaowafunda mara baada ya kupatikana” alisema Asha.
Wakati huohuo Kalala alisema kuwa anampongeza Asha kwa hatua hiyo aliyofikia na kwamba yeye ndiye atakuwa wa kwanza kukumbuka kuvumbua vipaji vya wapigaji wa ala za muziki.

“Hiki kitu mimi nilikuwa nakizungumzia kila siku kwani ni wanamuziki wachache sana ambao wanajua kuimba na kutumia ala wengi ni washika vipaza sauti tu mambo mengine hawajui mna hawawezi lakini hawajachelewa wanaweza kuanza sasa kwani elimu haina mwisho” alisema Kalala.

Kalala aliongeza kwa kusema kuwa yeye binafsi anamuunga mkono kutokana na kuja na wazo hilo jipya.

Tunaliheshimu wazo lake jipya alilokuja nalo na tutaitumia nafasi hiyo kwa kuwapa elimu wanamuziki chipukizi ili kuongeza tija kwa wapiga ala tofauti na ilivyo hivi sasa.

Mwisho ametoa wito kwa wazazi na walezi kuwapa ruhusa vijana wao kwenda katika usaili ,siku hiyo itakapofika.

Mbali ya kusaka wanamuziki watakaomudu kupiga ala pia watakaojitokeza watafundishwa kuimba na kucheza.

Wakati huohuo Asha aliongeza kwa kusisitiza kwamba wasanii wa mikoani nao wanahusika na zoezi linawahusu hivyo wajitokeze.
Asha Baraka akiwa na mmoja wa waalimu hao ambaye ni mwalimu katika Chuo Kikuu Huria Dar es Salaam wakiwa kati asehemu ya baadhi ya vyombo hivyo.

Post a Comment

0 Comments