Miss Tanzania 2011 Salha Esrael wakishirikiana na kipindi cha Njia mapema wiki hii wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo pampas,sabuni za maji,mashuka na vinginevyo ambavyo ni vitu muhimu kwa watoto wenye umri chini ya mwezi mmoja katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwenye Wodi ya Watoto namba 36 (Neonatal Ward).
Pichani Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akiwakabidhi baadhi ya vitu Manesi wa wodi hiyo maalum ya watoto kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Muhimbili.
Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akikabidhi pampas kwa ajili ya wodi hiyo maalum kwa watoto wnaozaliwa wakiwa chini ya umri wa mwezi mmoja,watoto hao ambao wamekuwa wakizaliwa hivyo kutokana na kukumbwa na matatizo mbalimbali.
Miss Tanzania 2011,Salha Esrael akimtazama mtoto wake ambaye ameamua kumuasili "kumuadapti" na kumpachika jina lake la Salha.Mlimbwende huyo,Salha kwa hivi sasa ameamua kujikita kwenye harakati za kutetea haki za watoto wachanga walio chini ya umri wa mwezi mmoja ambao kitaalamu wanaitwa Neonates, "watoto hawa wamekuwa wakisahauliwa kwa kiasi kikubwa,watu wanawakumbuka kuwasaidia watoto kuanzia miaka mitano na kuendelea,wanakimbilia kutoa vyandalua na mambo mengine,lakini ukweli ni kwamba kundi la watoto hawa limesahaulika mno,kwa hiyo kupitia Miss Tanzania 2011 tukishirikiana na kipindi cha Njia Panda tumetoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo pampas,sabuni za maji,mashuka na vinginevyo ambavyo ni vitu muhimu kwa watoto hawa ambao wamekuwa wakisahaulika siku hadi siku",alisema Salha.
Aidha Miss Tanzania 2011 Salha Esrael “amemuadapti” mtoto ambaye ni yatima mwenye umri wa chini ya mwezi mmoja na kumpa jina la Salha,mtoto huyo ambaye kwa sasa anaonakana kuendelea vyema kiafya alikutwa ametupwa vichakani na kuokotwa na wasamaria wema ambao walimfikisha haraka kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili,wodi ya watoto namba 36 (Neonatal Ward).Miss Tanzania 2011 Salha amebainisha wazi kuwa atahakikisha anamlea mtoto huyo katika maisha yake yote.
Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya kuvikabidhi vifaa hivyo kwa manesi wa wodi hiyo,Salha alisema kuwa yeye atajikita zaidi katika kutetea haki za watoto hao wachanga ambao wamekuwa
wakisahaulika kwa asilimia kubwa,ilhali watoto wengi wanaanzia kwenye hatua hiyo, “huu ni mwanzo tu wa kampeni hii,lakini nitakaporudi kwenye mashindano ya Miss Word yanayotarajiwa kufanyika hapo baadaye mwaka huu,mimi pamoja na wadau wengine tutahakikisha tunafanya kampeni kubwa ya kuihamasisha na kuielimisha jamii katika suala zima la kuwasaidia watoto hawa,ambao baadhi yao hutelekezwa na wazazi wao kutokana na kuwa na matatizo mbalimbali wangali wachanga”.
Mwendeshaji wa kipindi cha Njia Panda ambao ndio waratibu wa zoezi zima la ushiriki wa Miss Tanzania kutoa msaada kwenye wodi hiyo maalum,Dk. Isaac Maro akizungumza machache kuhusiana na tukio hilo.
Picha Zote na habarizimetumwa na Ahmad Issa Michuzi,(Michuzi JR)
P.O BOX 4156,
DAR ES SALAAM.
Phone:0713 422 313/ 0783 422 313
Tanzania- East Africa.
0 Comments