KAMPUNI YA BIA SERENGETI WAPANDA MITI 400 WILAYANI BAGAMOYO LEO

Kulia ni Meneja Mahusiano na Jamii Nandi Mwiliyombela akizungumza katika mkutano huo leo katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Magessa na Kocha wa Taifa Stars.Nandi amesema Kampuni ya Bia ya Serengeti imepanga kupanda miti 50,000 nchi nzima hivyo basi mara baada ya kupanda miti 400 Bagamoyo kesho watakwenda Mkoani Kilimanjaro na baadaye wataendeleza libeneke hilo katika mikoa mingine.Ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira duniani inayofikia kilele Juni 5 kila mwaka.

Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars wakisikiliza machache kuhusu mji wa Bagamoyo katika mkutano mfupi na Mkuu wa Wilaya Magessa Muhonho hayupo pichani, wilaya ya Bagamoyo ipo katika Mkoani Pwani .

Kocha wa timu ya Taifa Stars Poulssen akipanda mti leo wilayani bagamoyo.Poulsen amesema yeye anatambua umuhimu wa kutunza mazingira hivyo amewataka wakazi a eneo husika kuitunza miti hiyo 400 iliyopandwa na baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars ,Mkuu wa Wilaya na baadhi ya wafanyakazi wa SBL.

Mmoja wa Nyota wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Shaaban Kado akipanda mti leo Wilayani Bagamoyo ikiwa ni katika maandalizi ya kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani inayofikia kilele Juni 5 kila mwaka.Zoezi hilo limeandaliwa na Kampuni ya Serengeti (SBL).

Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wakiwa katika zoezi la upandaji miti hapa Mrisho Ngassa akimalizia ngwe yake ya kupanda mti.Wakiwa na Kocha wao Poulsen.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Magessa Muhongo akipanda mti katika zoezi hilo la kuelekea maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani inayoadhimishwa kila ifikapo Juni 5 .

Wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Serengeti wakiwa katika picha ya Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda miti 400 , katika neo la ofisi hiyo.

Post a Comment

0 Comments