MEYA DKT.NICAS ATOA SIKU SABA KUTOKOMEZA KERO YA NZI VISIGA



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dkt. Nicas Mawazo ametoa siku saba kwa Shamba la Kuku la lililopo Mtaa wa Madafu Kata ya Visiga Wilayani Kibaha kupulizia dawa ya kuua nzi ambao wamekuwa kero kwa wananchi  katika Kata hiyo.

Mhe.Mstahiki Meya Dkt. Nicas amsimamo huo baada ya wananchi kulalamikia shamba hilo kwenye  mkutano wa hadhara uliofanyika Mtaa wa Visiga Kati wakati akiwa kwenye ziara ya kutatua kero za wananchi kwenye Kata ya Visiga.

Sabra Selemani ambaye ni mwanach  amelalamika kuwa shamba hilo linalazisha Nzi kutokana na uchafu wa kinyesi cha kuku (mbolea) ambayo imekuwa ikikaa muda mrefu huoza na kuanza kutoa harufu mbaya.

Sabra amesema kuwa mbolea hiyo ikioza inazalisha funza ambao huzaa Nzi kwa wingi ambao husambaa kwenye baadhi ya Mitaa na kusababisha kero kubwa kwa wananchi hasa wale wanaofanya biashara za vyakula na wakati mwingine  huingia kwenye vyakula vyao hali inayowakimbiza wateja wao.
Haya ni baadhi ya mabanda ya kufuga kuku  katika shamba  Rasbery Farm. 
Msimamizi wa  Shamba la ufugaji  kuku Rasbery Farm  lililopo Visiga Kibaha  akiandaa dawa za kuulia Nzi mara baada ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dkt Nicas na Wataalam mbalimbali kutembeleana kukagua eneo hillo tarehe 02 Januari 2026.
Msimamizi wa shamba la kuku  CH. Prabhakaf akifafanua jambo  kuhusu kero  hiyo  na kuahidi kupiga dawa kuharibu  mazalia ya Nzi 

 Ameahidi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha  Dkt.  atakaporudi  hali itakua imebadilika.

Mstahiki Meya wa Manispaa  akielekea kwenye darasa la TEHAMA katika Shule ya Visiga.

Post a Comment

0 Comments