Super D anasema kuwa ameamua kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki katika kozi hiyo ambayo itahusisha makocha mbalimbali wa ngumi.
Amesema kuwa kozi hiyo itamsaidia kuongeza elimu juu katika mchezo wa ngumi na kuweza kuifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji vya vijana mbalimbali.´´
Nimeamua kuchukua fomu kwa ajili ya kushiriki katika kozi ya makocha ambayo itafanyika mwezi huu ambapo ninatarajia kuwa itanisaidia kuongeza ujuzi ikiwa ni pamoja na kuibua vipaji kwa vijana ambapo katika kozi hii nimedhaminiwa na Zulfiqar Ali.´´ alisema Super D.
0 Comments