Kikosi cha timu ya Uganda The Cranes watakaoshuka dimbani kukipiga na K'Jaro Stars.
Timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars leo inakumbana na kigingi kigumu cha kuvuka hatua ya nusu fainali ya michuano ya Chalenji pale itakapoumana mabingwa watetezi Uganda ‘The Cranes’ kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Stars imekata tiketi hiyo baada ya kuibanjua Rwanda ‘Amavubi’ bao 1-0 juzi, likifungwa na nahodha wake Shadrack Nsajigwa ‘Fusso’, huku The Cranes ikiiondosha Zanzibar ‘Zanzibar Heroes kwa penalti 5-3, baada ya kwenda sare ya 2-2 dakika 90.
Mechi ya leo inatarajiwa kuwa ngumu, kutokana na ubora wa timu zote, huku pia kila moja ikitaka kushinda ili kutinga fainali ya michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Novemba 27.
Hata hivyo, Stars ina nafasi ya kushinda mechi hiyo hasa ikizingatiwa inacheza uwanja wa nyumbani sambamba na kupata sapoti ya kutosha kutoka kwa mashabiki wake.Aidha kocha mkuu wa Stars Jan Poulsen, amekuwa akirekebisha kasoro za kikosi chake kila baada ya mchezo, hali inayokifanya kizidi kuwa bora zaidi kadiri siku zinavyosonga.Lakini, Stars inapaswa kuwa makini zaidi katika mchezo wa leo, kwani itakumbana na nyota wengi ambao wanalifahamu soka la Tanzania na mazingira yake.
Nyota wa Uganda ambao wanacheza hapa nchini na wanatarajiwa kutoa upinzani mkubwa leo ni pamoja na mshambuliaji mahiri wa Simba, Emmanuel Okwi, winga Dan Wagaluka ambaye msimu uliopita alikuwa Azam FC na beki Ibrahim Shikanda ambaye bado yuko na Wauza Koni hao.
Wengine ni beki George Owino na kiungo Patrick Ochan wanaokipiga Simba na Steven Bengo aliyekuwa Yanga msimu uliopita. Mechi hiyo na nusu fainali ya kwanza kati ya Ivory Coast na Ethiopia.
Fainali za michuano hiyo zitafikia tamati keshokutwa, ambako mshindi atazawadiwa dola 30,000, mshindi wa pili atapata dola 20,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa dola 10,000.

0 Comments