Mabadiliko makubwa katika ushirikishwaji wadau wa sekta ya utalii yameibuliwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro ikianza mwanzo wa safari mpya ya simulizi kwa chapa ya Destination Ngorongoro kwa kuzungumza sauti moja, iliyo thabiti, yenye kujiamini na kukumbukwa imeamua kuzindua shindano la picha lijulikanalo kama “The Birth of Wonders photo competition” litakalohusisha waongoza watalii katika eneo la Ndutu katika msimu huu wa mazalia ya Nyumbu.
Akitangaza kampeni hiyo Kamishna Msaidizi Mwandamizi anayesimamia huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo ameeleza kuwa shindano hilo linahusu eneo la Ndutu ambapo ndipo Safari Kuu ya Nyumbu huzaliwa na maisha kuanza ambapo eneo hilo hadithi ya Ngorongoro hujirudia upya kila mwaka.
“Waongoza Watalii ni mabalozi wetu muhimu katika kuisimulia Ngorongoro kwa dunia, katika msimu huu wa uzaaji wa nyumbu hapa Ndutu, tunawaalika kutumia lenzi zao kunasa Pumzi za kwanza za uhai wa ndama, Hatua za kwanza za ndama, Mahusiano ya mama na mwana,
Waongoza kupiga picha na kuzituma kupitia akaunti zao za instagram, _tag_ na kushiriki (collaborate) na akaunti rasmi ya _instagram_ ya ngorongoro (@visitngorongoro
Katika shindano hilo la upigaji picha ( _The Birth of Wonders photo competition)_ Washindi watachaguliwa kwa kuzingatia ushiriki (engagement) wa watazamaji pamoja na kufuata masharti yote ya shindano ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita kinono cha shilingi Milioni 3,000,000, mshindi wa pili shilingi milioni 2,000,000 na mshindi wa tatu atajishindia milioni 1,000,000 mtawalia.
Waongoza Watalii ambao ni washiriki wa kampeni hii wanakuwa wasimulizi wa sauti ya chapa ya Destination Ngorongoro Kwani wao ndiyo mashuhuda wa kwanza wa simulizi ya uzao wa nyumbu.





0 Comments