ALIYEKUWA Mwenyekiti wa
Bongo Movie, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema yeye ni sawa na aliyekuwa
Rais wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, kwani tangu uongozi wake ulipopinduliwa
na kuuawa, nchi hiyo haijaweza kutawalika na hivyo ndivyo ilivyo kwa Bongo
Movie pichani juu.
Steve Nyerere alisema
anajifananisha na Gaddafi kwa sababu moja kuu, kwanza aliweza kuwakutanisha
wadau mbalimbali na wasanii wa Bongo Movie, ikiwemo viongozi mbalimbali wa
serikali.
“Lakini mara baadhi ya wanachama
wa Bongomovie walipoanza kuleta majungu, nikaamua kujiuzulu na hadi sasa hakuna
tena umoja huo, umebakia historia kama ilivyobaki historia ya nchi ya Libya
kuwa, wananchi wake waliishi kwa raha mustarehe katika enzi za utawala wa Gaddafi
na sasa hakutawaliki, hakukaliki, ndivyo ilivyo kwa umoja huu wa hapa nchini
umesambaratika, yote ni kwa sababu ya roho mbaya na choyo, waliona mimi
nafaidika sasa mbona wanashindwa kujitawala,” alihoji Nyerere.
Nyerere alitwaa nafasi hiyo
katika uchaguzi uliofanyika mapema mwaka jana, lakini balaa lilikuja kumkumba
katika kashfa ya uzinduzzi wa filamu na kudaiwa kula fedha za mfuko wa PSPF ,
tuhuma alizozikanusha vikali na kuamua kuachia ngazi ya uongozi wa Bongo Movie Unity Septemba mwaka
jana na hadi sasa hakuna kiongozi yeyote aliyerithishwa mikoba wala kuitishwa
uchaguzi tangu ang’atuke.
0 Comments